• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (4 Julai-8 Julai)

  (GMT+08:00) 2016-07-08 19:12:25

  Maafisa wanne wa polisi wauwa mjini Dallas, Marekani

  Maafisa wanne wa polisi mjini Dallas, Marekani wamepigwa risasi na kuuawa wakati wa maandamano ya kupinga mauaji ya watu weusi.

  Maafisa wa polisi katika mji ulio katika jimbo la Texas, wanasema mauaji hayo yametekelezwa na washambuliaji wawili wa kulenga shabaha.

  Maafisa wengine saba wa polisi wamejeruhiwa, Bw Brown amesema.

  Wawili wamefanyiwa upasuaji wa dharura na mmoja yumo katika hali mahututi.

  Ufyatuaji risasi ulianza waandamanaji walipokuwa wakipitia barabara za mji na kuwafanya waandamanaji kukimbilia usalama wao.

  Maandamano hayo yalitokana na kuuawa kwa wanaume wawili weusi, Philando Castile jimbo la Minnesota na Alton Sterling eneo la Baton Rouge jimbo la Louisiana.


  1 2 3 4 5 6 7 8 9 10
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako