• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (4 Julai-8 Julai)

    (GMT+08:00) 2016-07-08 19:12:25

    Narendra Modi azuru Msumbiji

    Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ameanza ziara yake barani Afrika, wiki hii akianzia nchini Msumbiji. Kabla ya kuanza ziara hii, Waziri Mkuu Modi amedokeza kuwa anakuja barani Afrika kutoa ujumbe kuwa India ni rafiki wa kuamini.

    Nchini Msumbiji amekutana na rais Filipe Nyusi jijini Maputo na kutoa saini mikataba kadhaa ya ushirikiano wa kibiashara kati ya mataifa hayo mawili.

    Wachambuzi wa maswala ya uchumi wanasema ziara ya Modi ni kuyashawishi mataifa ya Afrika kushirikiana na nchi yake zaidi latika maswala mbalimbali lakini pia kuonesha kuwa inaweza kushinda na China ambayo inaonekana kukita mizizi katika matifa mbalimbali ya Afrika na kufadhili miradi kama ya ujenzi wa reli ya kati nchini Kenya na barabara.

    Mbali na Msumbiji, Waziri Mkuu huyo atazuru Afrika Kusini, Tanzania na hatimaye nchini Kenya.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako