• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (4 Julai-8 Julai)

    (GMT+08:00) 2016-07-08 19:12:25

    Uingereza inatarajiwa kuwa na Waziri Mkuu mwanamke, wa kwanza baada ya Waziri Mkuu wa zamani Margaret Thatcher. Hii ni mara ya pili Uingereza kuwa na Waziri Mkuu mwanamke katika historia yake

    Hili limebainika baada ya chama tawala cha Conservative kuwachagua wanasiasa wawili wanawake, Theresa May na Andrea Leadsom kuwania wadhifa huo baada ya Waziri Mkuu wa sasa David Cameron kutangaza kuwa atajiuzuliu kabla ya mwezi Oktoba baada ya raia wa Uingereza kuamua kujiodnoa kwenye Umoja wa Ulaya.

    Wawili hao sasa watapambana kuwania Uenyekiti wa chama chao kwa kupigia kura na zaidi ya wajumbe 150,000 na mshindi atatangazwa tarehe 9 mwezi Septemba.

    Theresa May ni Waziri wa Mambo ya ndani huku Andrea Leadsom akiwa Naibu Waziri katika Wizara ya Nishati.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako