• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (4 Julai-8 Julai)

    (GMT+08:00) 2016-07-08 19:12:25

    Sudan Kusini kuadhimisha miaka 5 ya uhuru

    Sudan Kusini inaadhimisha miaka mitano ya Uhuru wake Jumamosi hii wakati ambapo hali ya usalama inaonekana tulivu katika baadhi ya maeneo, lakini mapigano yamekua yakirindima katika mji wa Wau.

    Hata hivyo, serikali ya Juba tayari imetangaza kuwa hakutakuwa na shamrashamra zozote hapo kesho lakini rais Salva Kiir atalihotubia taifa.

    Ni miezi michahache tu baada ya nchi hiyo kuanza kushuhudia amani baada ya Rais Kiiir na aliyekuwa kiongozi wa waasi Riek Machar kuanza kushirikiana kuongoza serikali ya mpito.

    Nchi hiyo kwa sasa inakabiliwa na chanagamoto za kifedha baada ya miaka miwili ya mapigano lakini mapigano mapya yameripotiwa katika mji wa Wau hivi karibuni.

    Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini kimesema kwamba kumekuwa na milio ya risasi zaidi katika mji wa kaskazini magharibi wa Wau.

    Inaarifiwa kwamba takriban watu laki mbili unusu wameyahama makazi yao na kukimbilia kwenye maeneo salama.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako