Wafanyakazi wa UN washambuliwa Nigeria
Washambuliaji wasiojulikana wameshambulia msafara wa Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, katika jimbo la Borno nchini Nigeria.
Wafanyakazi kutoka katika mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa UNICEF, IOM na UNFPA walikuwa wakitokea Bama kwenda Maiduguri katika jimbo hilo la Borno, ambako waligawa misaada ya kibinadamu
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF, mfanyakazi mmoja wa shirika hilo na mwingine kutoka IOM walijeruhiwa katika shambulio na kukimbizwa hospitali.
Msafara huo ulikuwa katika maeneo ya mashambani kaskazini mashariki mwa Nigeria, ambako mizozo ya wenyewe kwa wenyewe imesababisha kuwepo kwa tatizo la utapiamlo.
Kwa mujibu wa UNICEF shambulio hilo sio tu limewagusa wafanyakazi hao wa kutoa misaada, bali pia watu wote wanaohitaji misaada na usaidizi unaoletwa na watu hao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |