• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (23 Julai-29 Julai)

    (GMT+08:00) 2016-07-29 18:56:28

    Jeshi la DRC laanza operesheni dhidi ya kundi la wapiganaji wenye silaha

    Jeshi la ulinzi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC limeanza operesheni ya kijeshi iitwayo "Kiboko 3" dhidi ya kundi la FRPI mashariki mwa nchi hiyo.

    Msemaji wa jeshi hilo Jenerali Leo Kasonga amesema, lengo la operesheni hiyo ya kijeshi ni kuwashinda wapiganaji wa kundi la FRPI ambao wameanza tena kufanya mashambulizi dhidi ya raia.

    Jenerali Kasonga amesema, kundi hilo halina nguvu, lakini uwepo wa baadhi ya wapiganaji wake katika eneo hilo na kuendelea kwa wizi wa mifugo kutoka kwa wakazi wa eneo hilo, kunahatarisha uwezekano wa kutokea mapigano ya kikabila kati ya watu wanaoishi kwa amani kwenye kanda hiyo.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako