• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (23 Julai-29 Julai)

    (GMT+08:00) 2016-07-29 18:56:28

    Salva Kiir amuapisha Jenereli Taban Deng Gai kuwa Makamu wa wa rais

    Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir wiki hii amemuapisha Jenereli Taban Deng Gai kuwa Makamu wa kwanza wa rais kuchukua nafasi ya Riek Machar ambaye aliondoka jijini Juba mapema mwezi huu baada ya kuzuka kwa mapigano mapya.

    Hatua hii inadhirisha wazi mgawanyiko kati ya wanasiasa wa upinzani wa SPLM-IO wanaoongozwa na Machar ambaye hajulikani aliko.

    Brigidia Taban Deng ambaye ni waziri wa madini amechaguliwa baada ya kikao cha wapinzani wa wa Machar katika kundi la Sudan People's Liberation Movement in-Opposition (SPLM-IO) ambao vinara wao wanapingwa na wafuasi wa Machar.

    Bw Deng alikuwa mpatanishi mkuu wa Machar na hatua yake ya kuchukua wadhifa huo inaonyesha kuwa wametofautiana sana, hivyo basi kuweka mgawanyiko katika upinzani jambo ambalo linazidi kutatiza juhudi za kupata amani nchini Sudan Kusini.

    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako