• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (23 Julai-29 Julai)

    (GMT+08:00) 2016-07-29 18:56:28

    Rais wa Syria atoa msamaha kwa waasi watakaojisalimisha ndani ya miezi mitatu

    Rais Bashar al-Assad wa Syria ametoa amri ya kuwasamehe waasi wenye silaha watakaojisalimisha ndani ya miezi mitatu.

    Shirika la habari la taifa la Syria SANA limesema, amri hiyo inahusisha mtu yeyote anayemiliki silaha kwa sababu yoyote, kama watajisalimisha kwa mamlaka husika ndani ya miezi mitatu kuanzia leo.

    Pia katika msamaha huo, rais Assad ameahidi kuwasamehe watekaji nyara ambao watawaachia huru mateka bila ya kuwadhuru na bila kudai fedha.

    Habari nyingine zinasema, jeshi la serikali ya Syria na wapiganaji wanaoliunga mkono jeshi hilo wamedhibiti ngome muhimu ya waasi mjini Aleppo.

    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako