• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (23 Julai-29 Julai)

    (GMT+08:00) 2016-07-29 18:56:28

    Rwanda yateketeza tani 55 za silaha

    Rwanda imeteketeza zaidi ya tani 50 za silaha zisizohitajika na zilizoharibika.

    Zoezi hilo linaongozwa na jeshi la ulinzi la Rwanda RDF kwa kushirikiana na kituo cha udhibiti wa silaha ndogondogo cha Maziwa Makuu, pembe ya Afrika na nchi zinazopakana RECSA, na linalenga kuisaidia Rwanda kuondoa silaha zenye hatari na kuzuia uhalifu.

    Kazi ya kutekeleza silaha ni ya kawaida nchini Rwanda tangu mwaka 1994.

    Baada ya zoezi hilo, katibu mtendaji wa RECSA Theoneste Mutsindashyka amesema silaha hizo zingesababisha hatari kubwa.

    Uhifadhi wa silaha zilizopita muda wake umekuwa ukisababisha ajali katika nchi mbalimbali za Afrika. Mwaka 2011 watu 26 walikufa nchini Tanzania baada ya zilaha zilizokwisha muda wake kulipuka. Mwaka uliofuata watu 200 walikufa baada ya jalala la silaha mjini Brazzaville lilipolipuka na kusababisha vifo vya watu 200.

    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako