• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( Septemba 3-Septemba 9)

  (GMT+08:00) 2016-09-09 19:50:28
  Jean Ping wa Gabon akata rufaa

  Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Gabon, Jean Ping, amekata rufaa kwenye mahakama ya katiba kupinga matokeo ambapo amesema aliibiwa kura kwenye uchaguzi wa mwezi uliopita.

  Rais aliyekuwa madarakani Ali Bongo alishinda kuendelea kuongoza nchi hiyo kwa kura chini ya elfu sita.

  Ping hakubaliani na matokeo kutoka kwa ngome za bwana Bongo ambapo yeye alishinda kwa zaidi ya asilimia 95 ya kura zote ambapo waliopiga kura walikuwa ni asilimia 99.93.

  Waangalizi wa umoja wa ulaya nao wamekosoa matokeo kwa baadhi ya majimbo.

  Bwana Ping amesema watu kadhaa wameuawa kwenye vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi , lakini serikali imesema kuwa ni watatu pekee ndiyo waliuawa.

  1 2 3 4 5 6 7 8
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako