• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 29-Februari 2)

  (GMT+08:00) 2018-02-02 20:05:30

  AU yakamilisha mkutano wake Addis

  Mkutano wa wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika umekamilika mapema wiki hii mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

  Wakuu hao wa bara Afrika walianza kukutana mwishoni mwa wiki iliyopita, kujadili masuala mbalimbali yanayowasumbua waafrika kama ukosefu wa usalama na uchumi.

  Kauli mbinu ya mwaka 2018 wa Umoja huo ni namna ya kupambana na ufisadi.

  Rais wa Nigeria Muhamadu Buhari amepewa jukumu la kusimamia juhudi za kupambana na ufisadi.

  Buhari tangu kuchaguliwa kwake mwaka 2015, amekuwa akisfiwa sana katika vita dhidi ya ufisadi katika nchi yake.

  Mwenyekiti mpya wa Umoja huo rais wa Rwanda Paul Kagame, ametoa wito kwa wakuu wa nchi za Afrika kufungua mipaka yake, ili kuwaruhusu waafrika kutembea bila vikwazo.

  Rwanda imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika, kuondoa vikwazo vya kuingia nchini mwake kwa lengo la kuhimiza Umoja wa Afrika. AU inataka kuondoa mipaka na kuungana kisiasa kufikia 1963.

  Aidha, Kagame anataka teknolojia kutumiwa vema ili kusaidia kuunda nafasi za kazi hasa kwa vijana.

  Suala la namna bara la Afrika linavyoweza kujitegemea kwa kupata fedha zake bila ya kutegemea misaada kutoka mataifa ya nje.

  Mbali na viongozi wa Afrika, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress na kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas wamehudhuria mkutano huo.

  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako