• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 29-Februari 2)

    (GMT+08:00) 2018-02-02 20:05:30

    Somalia na Umoja wa Mataifa zazindua mpango wa kuboresha maisha ya wakimbizi wa ndani

    Somalia na Umoja wa Mataifa zimezindua mpango wa uvumbuzi wa kukusanya mapendekezo kutoka kwa vijana wa Somalia kuhusu kuboresha hali ya maisha ya wakimbizi wa ndani nchini Somalia.

    Maofisa wa serikali ya Somalia na Umoja wa Mataifa wanaohudhuria uzinduzi wa mpango huo, wanawahimiza vijana wa Somalia kutoa utatuzi kwa ajili ya matatizo mbalimbali yanayowakabili wakimbizi wa ndani nchini mwao.

    Mkurugenzi wa Shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP Bw. Achim Steiner amewashauri vijana wa Somalia kuendeleza mitandao ya kitaaluma kukuza uvumbuzi wao.

    Mpango huo ni sehemu ya mradi wa "uvumbuzi kwa Somalia" unaoongozwa na UNDP kwa kushirikiana na serikali ya Somalia, ili kukabiliana na changamoto mbili zinazopewa kipaumbele katika kuboresha sekta za maziwa na app za simu za mkononi za kuhimiza maendeleo.

    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako