• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 29-Februari 2)

  (GMT+08:00) 2018-02-02 20:05:30

  Maelfu ya raia wahama makazi yao kufuatia mapigano mashariki mwa DRC

  Mapigano yanayoendelea kusini mwa mkoa wa Kivu kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamesababisha wimbi kubwa la wakimbizi katika nchi jirani za Burundi na Tanzania.

  Maelfu ya watoto, wanawake na wanaume wameacha makazi yao huku mapigano dhidi ya makundi yenye silaha ya Mai Mai yakiendelea Kusini mwa mkoa wa Kivu.

  Mapigano makali yanaendelea katika kisiwa cha Ubwari.

  Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR limesema limeshtushwa na mapigano yanayoendelea Mashariki mwa Demokrasia ya Congo, ambayo yamesababisha wimbi kubwa la wakimbizi kutoka nchini humo wanaoingia katika nchi za Burundi, Tanzania na Uganda.

  Kwa mujibu wa Shirika hilo, mpaka sasa, wakimbizi wapatao 1200 wameingia nchini Tanzania. Wakati huo huo, inaamika kwamba,

  UNHCR inabaini kwamba kuna wakimbizi wengi ambao wamekwama katika maeneo yenye mapigano, ambao ewako katika hali mbaya ya kukosa chakula na makazi.

  Bi Joan Allison naibu mwakilisha wa UNHCR nchini Tanzania amesema kuwa wakimbizi 1200 wameingia nchini Tanzania na wamesafirshwa katika kambi ya Nyarugusu.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako