• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 29-Februari 2)

  (GMT+08:00) 2018-02-02 20:05:30

  Mawaziri wakuu wa China na Uingereza wazungumza na wajasiriamali kutoka nchi hizo mbili

  Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang na waziri mkuu wa Uingereza Bi. Theresa May ambaye wiki hii amekuwa ziarani nchini China wamehudhuria hafla ya kuanzisha Kamati ya Wajasiriamali kutoka China na Uingereza na kuzungumza na wajumbe wao.

  Bw. Li Keqiang amesema, hivi sasa uchumi wa dunia unafufuka, kuanzishwa kwa Kamati hiyo kutaimarisha zaidi ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

  Bi. May amesema, baada ya kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya, Uingereza itaendelea kufungua mlango, na Uingereza na China zinatarajiwa kuanzisha uhusiano wa karibu zaidi wa kiuchumi na kibiashara.

  Wajasirimali kutoka kampuni zaidi ya 30 za nchi hizo mbili zinazojikita katika mambo ya fedha, nishati, mawasiliano ya simu, magari, dawa na usafiri wamefanya majadiliano ya kina kuhusu masuala ya biashara, uwekezaji, soko huria, na ushirikiano wa uvumbuzi.

  Baadaye pia Theresa May alikutana na Rais Xi Jinping wa China ambapo Rais Xi amezitaka nchi hizo mbili kufanya kazi kwa pamoja kwa ajili ya maendeleo ya utulivu ya uhusiano wa pande mbili katika zama mpya.

  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako