• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 29-Februari 2)

  (GMT+08:00) 2018-02-02 20:05:30

  UNICEF yasema watoto 378,000 wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu katika mwaka 2018

  Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto (UNICEF) limethibitisha kwamba, baada ya miaka saba ya vita, hali ya kibinadamu nchini Libya inaendelea kuzorota na watoto 378,000 wanahitaji ulinzi na msaada wa haraka wa kibinadamu.

  Mwakilishi maalum wa UNICEF nchini Libya Bw. Abdel Rahman Ghandour amesema, Shirika hilo linaomba dola za kimarekani milioni 20 ili kusaidia kuimarisha msaada wa kuokoa maisha na kuwasaidia watoto nchini Libya ambao wanastahili kuwa na maisha mazuri ya baadaye.

  Mwaka huu, UNICEF ina lengo la kuwapa watoto wa Libya msaada wa matibabu na kisaikolojia, elimu, ulinzi, usafi wa mazingira na huduma za maji, na kuendelea na kazi za kuunga mkono mpango wa msaada wa kinadamu na kurejesha wafanyakazi na washirika nchini Libya.

  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako