• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 29-Februari 2)

    (GMT+08:00) 2018-02-02 20:05:30

    Kenya kuanza uchunguzi kuhusu kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani

    Kenya imeendelea kuwa na utulivu baada ya muungano wa upinzani NASA kumwapisha kiongozi wake Bw. Raila Odinga kuwa "rais wa watu" kwenye sherehe fupi iliyohudhuriwa na maelfu ya watu katika uwanja wa Uhuru mjini Nairobi.

    Baada ya kuapishwa kwake Bw Odinga alisema atapigania demokrasia zaidi, usawa na utawala bora nchini Kenya

    Serikali sasa imeanza uchunguzi kuhusu sherehe ya kuapishwa kwa Bw Raila Odiga.

    Waziri wa mambo ya ndani na uratibu wa serikali kuu Bw. Fred Matiang'i amesema uchunguzi huo utawahusu washiriki na waliofanikisha tukio hilo.

    Amesema baada ya uchunguzi kukamilika, hatua stahiki zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria za Kenya. Bw. Matiang'i amesema hayo baada ya polisi kumkamata mbunge wa upinzani Bw. Tom Kajwang aliyemwapisha Bw Odinga kwenye shughuli iliyofanyika kwa amani na kuhudhuriwa na maelfu wa waungaji mkono wa upinzani.

    Bw. Matiang'i pia amesema serikali inajua baadhi ya vyombo vya habari vilivyoshiriki kwenye tukio hilo na kupuuza agizo la serikali na wajibu wao kwa usalama wa Kenya, na vyombo hivyo vitaendelea kufungwa hadi uchunguzi utakapokamilika.

    Wakati huo huo Polisi nchini Kenya walifanya uchunguzi kuhusu watu wasiojulikana kurusha guruneti na kufyatua risasi katika nyumba ya kiongozi wa upinzani na aliyekuwa makamu wa rais wa nchi hiyo, Kalonzo Musyoka usiku wa jana.

    Kamanda wa polisi wa wilaya ya Karen Cunnigham Suiyanka amethibitisha tukio hilo, akisema hakuna mtu aliyejeruhiwa katika shambulizi hilo.

    Wapelelezi kutoka kitengo cha mabomu wamepelekwa nyumbani kwa kiongozi huyo ambaye pia ni mmoja wa viongozi wa muungano wa upinzani wa NASA, unaoongozwa na Raila Odinga.

    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako