• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 29-Februari 2)

  (GMT+08:00) 2018-02-02 20:05:30

  Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa laongeza vikwazo dhidi ya

  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio kuhusu kuongeza muda wa vikwazo dhidi ya wanaoharibu amani na utulivu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR kwa mwaka mmoja zaidi hadi Januari 31 mwaka 2019.

  Baraza hilo limepitisha azimio namba 2399 likizitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuendelea kuchukua hatua za lazima, ili kuepusha kutoa, kuuza au kusafirisha silaha na vifaa husika kwa CAR, na kuepusha kutoa msaada wa teknolojia husika, fedha na mafunzo kwa nchi hiyo.

  Marufuku ya usafirishaji wa silaha hayatakihusu kikosi cha ulinzi wa amani cha Umoja huo nchini CAR na ujumbe wa utoaji wa mafunzo kutoka Umoja wa Ulaya.

  Kwa mujibu wa azimio hilo, kamati ya vikwazo itaendelea kutekeleza marufuku ya usafirishaji na kuzuia mali za watu au mashirika yanayotambuliwa kushiriki au kuunga mkono shughuli za kuharibu amani, utulivu na usalama wa CAR hadi Januari 31 mwaka kesho.

  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako