• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • • Mwitikio wa wananchi wa China kuhusu sera ya kuwa na watoto wawili
    Ni mwaka mmoja sasa tangu sera ya kuwaruhusu wanandoa kuwa na mtoto wa pili kama mmoja kati yao ni mtoto wa pekee katika familia ianze kutekelezwa katika mikoa mbalimbali nchini China. Lakini hali halisi ni kuwa, ombi la kuzaa mtoto wa pili halikuongezeka kwa kiasi kikubwa kama wachina walivyotarajia.
    • Maendeleo yaliyopatikana katika mambo ya wanawake nchini China na katika nchi za Afrika Mashariki
    Habari kutoka Mkutano wa kwanza wa Kamati ya 6 ya wafanyakazi wanawake ya Shirikisho kuu la wanawake la CHina zimesema, hadi sasa idadi ya jumla ya wafanyakazi wa kike imefikia milioni 137, kiasi hicho kinachukua asilimia 40 ya idadi ya jumla ya wafanyakazi nchini China. Mbali na hayo, kiwango cha elimu cha wanawake pia kimeinuka kwa udhahiri. Kwa mfano idadi ya wafanyakazi wanawake waliopata elimu ya chuo kikuu inachukua asilimia 51.9 ya idadi ya jumla ya wafanyakazi, kiasi hicho kimeongezeka kwa asilimia 34.6 kuliko miaka mitano iliyopita.
    • Hisia tofauti kuhusu ulipaji wa mahari
    Nchini Kenya kiongozi wa kanisa la Katoliki Kadinali John Njue, anatoa wito kwa wazazi kulegeza kamba katika ulipaji mahari kabla ya harusi kufanyika, ili kusaidia vijana wengi kuoa.
    Lakini hoja hiyo imeanza kuzua hisia tofauti miongoni mwa wakenya, haswa ikizingatiwa kwamba mila na desturi za kiafrika katika maswala ya ndoa, zinahusu utoaji wa mahari kwanza kabla ya msichana kuolewa.
    • Sera ya China kuhusu watoto wawili yafuatiliwa na watu
    Sera ya uzazi wa mpango ni sera muhimu hapa China. Kadiri hali ya uchumi na jamii inavyozidi kupata maendeleo, ndivyo sera hiyo inavyozidi kurekebishwa na kukamilika. Hivi karibuni serikali ya China imetangaza kutekeleza sera ya watoto wawili kwa familia ambayo mmoja kati ya wanandoa ni mtoto wa pekee katika familia yake. Sera hiyo imethibitishwa katika Mkutano wa tatu wa Kamati kuu ya 18 ya chama cha Kikomunisti cha China uliofanyika mwezi uliopita na katika Mkutano wa 6 wa baraza la 12 la kudumu la bunge la umma la China uliofanyika tarehe 23 Desemba mjini Beijing.
    • Maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa watoto yapungua kwa asilimia 50 katika nchi saba zilizoko kusini mwa Sahara
    Ripoti mpya iliyotolewa hivi karibuni imeonesha kuwa, tangu mwaka 2009 maendeleo makubwa yamepatikana katika kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI kwa watoto wa Afrika, huku nchi saba zilizoko kusini mwa Sahara zikiwa zimepunguza kiwango cha maambukizi kwa asilimia 50.
    • China yaendelea na mchakato wa kutunga sheria ya kuzuia vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake
    Katika miaka mitano iliyopita baraza la 11 la bunge la umma la China, limekuwa likitoa miswada na mapendekezo kuhusu kuzuia vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake ambayo yamekuwa yakiongezeka, na mengi zaidi yanahusu kuzuia vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake nyumbani, unyanyasaji wa kijinsia, pamoja na kupambana na uhalifu wa kuuza wanawake na watoto.C. Kamati ya wafanyakazi katika Halmashauri ya kudumu ya bunge la umma la China pamoja na kamati maalumu inayohusika mara nyingi zimekuwa zikifanya utafiti kuhusu kazi ya kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake nyumbani. Kutokana na juhudi za pamoja za pande mbalimbali, kazi ya kutunga sheria katika mambo hayo imepata maendeleo makubwa.
    • Desturi ya kutoa bahasha nyekundu kwa watoto imebadilika kuwa mzigo kwa watu
    Sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China imemalizika hivi karibuni, katika sikukuu hii kuna desturi moja ya kuwapa watoto bahasha nyekundu ambayo ndani yake mna fedha taslim kwa mfano " mtoto mmoja wa kiume alipewa bahasha nyekundu zenye pesa elfu 20 ndani ya siku saba", na "mfanyakazi mmoja wa kampuni moja alitoa bahasha nyekundu 46 wakati wa sikukuu hiyo". Hivyo suala hili la kutoa bahasha nyekundu linafuatiliwa sana na watu kila baada ya kumalizika kwa sikukuu ya mwaka mypa wa jadi wa China.
    • Jinsi hali ya umaskini unavyowakabili wanawake hususan vijijini barani Afrika kuliko wanaume
    Hivi sasa wanawake wengi wa vijijini hususan katika bara la Afrika wamekuwa wakijihusisha shughuli za kilimo cha mazao ya chakula na shughuli zinazowapatia kipato kidogo, wakati wanawake maskini waishio mijini waliendesha biashara ndogo ndogo katika sekta isiyo rasmi. Je, chanzo cha hali hiyo ni nini? Na wanawake hao wanatakiwa kufanya nini ili kubadilisha hali hiyo? Kipindi hiki cha Sauti ya Wanawake kitazungumzia suala hili.
    • Ushirikishwaji wa wanawake kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo
    Kwa muda wa miongo kadhaa iliyopita, wanawake wametokea kuwa ni wenye juhudi kubwa katika masuala ya jamii zao. Lakini hadi sasa bado wangali mbali sana na mahali ambapo wangestahili kuwa, iwe ni katika sekta binafsi au ya umma. Hali hii inatokana na ukosefu wa usawa wa jinsia ambao unaendelea kusababisha matatizo mengi barani Afrika na hata duniani. Wanawake wanaponyimwa haki zao za msingi zikiwemo kufanya maamuzi au kukoseshwa udhibiti wa raslimali kama vile ardhi na nyinginezo, wanashindwa kuleta maendeleo kuanzia ngazi ya familia hadi taifa. Lakini ni vyema tukajiuliza kwanini hadi leo baadhi ya tamaduni zinamzuia mwanamke kushiriki moja kwa moja katika kuleta maendeleo, au kwanini fursa za elimu hazitolewi kwa usawa kati ya mwanamke na mwanamume?
    • Ripoti ya kwanza ya utafiti kuhusu mahitaji ya watoto wa China kwa misaada yatangazwa
    Ripoti ya kwanza ya utafiti kuhusu mahitaji ya watoto wa China kwa misaada ya mwaka 2012 imetolewa hivi karibuni mjini Beijing, China. Ripoti hiyo inaandaliwa kwa pamoja na Mfuko wa watoto na vijana wa China, pamoja na kituo cha utafiti wa misaada ya jamii katika Chuo cha maendeleo ya jamii na sera za umma cha Chuo Kikuu cha Ualimu cha Beijing baada ya kufanya utafiti kuhusu mashirika 45 yanayoshughulikia mambo ya watoto katika miji na mikoa 13 kote nchini China.
    • Je, ni bora kuolewe na mtu tajiri au kujitahidi binafsi na kupata mafanikio?
    Kadiri siku zinavyoenda ndivyo mambo yanavyobadilika, siku hizi tunakuta mwanamke atafute mtu tajiri aolewe naye ili apate kila kitu, lakini akisema hangaike mwenyewe hapendi, sasa swali limekuja, je, ni bora kuolewe na mtu tajiri au kujitahidi binafsi na kupata mafanikio, kipindi hiki cha Sauti ya Wanawake kitazungumzia suala hilo.
    • Mama wa namna gani atakayemlea mtoto wake vizuri?
    Hivi karibuni kitabu kinachoitwa Battle Hymn of the Tiger Mother kimeleta athari kubwa katika sekta ya elimu nchini Marekani, na kuanzisha majadiliano kuhusu njia zipi watakazozitumia mama kuwaelimisha watoto kati ya China na Marekani. Katika kipindi hiki cha Sauti ya Wanawake mwandishi wetu wa habari amewahoji wakinamama kadhaa wa China kuhusu maoni yao juu ya kitabu hicho, na mbinu za za kuwalea watoto..
    • "Mahodhi ya kuhifadhia maji"
    "Mahodhi ya kuhifadhia maji" ni mradi mmoja wa kutoa huduma za maji. Ulianzishwa na Mfuko wa maendeleo ya wanawake ya China mwaka 2001, lengo lake ni kuwasaidia wakazi waliokaa kwenye sehemu ya magharibi nchini China hususan wanawake wajiondoke kutoka hali duni kutokana na tatizo la ukosefu wa maji. Hadi sasa kwa ujumla wamenufaisha watu zaidi ya milioni 1.7. Hivi karibuni mwandishi wa habari Pili Mwinyi ametembelea mkoa huo, na kushuhudia jinsi mahodhi ya aina hiyo yanavyofanya kazi. Kipindi hiki cha Sauti ya Wanawake kitazungumzia hali halisi kuhusu mradi huo.
    Mbali na hayo, kipindi hiki pia kitazungumzia saratani ya matiti, na namna ya kutunza uso wakati wa kuwa njiani kwenye pilikapilika za kila siku.
    prev 1 2 3 4
    SearchYYMMDD  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako