• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • • Hatua zinazochukuliwa kukinga na kudhibiti ukimwi kwa wanafunzi wa vyuo na shule za China
    Katika miaka ya hivi karibuni, idadi ya wanafunzi vijana wa China wanaoambukizwa ukimwi imeongezeka. Hii inatokana na baadhi ya shule kutofanya vizuri kazi ya kuwaelimisha wanafunzi hao namna ya kujikinga na ukimwi, na vilevile udhaifu wa mawazo ya wanafunzi hao katika kujilinda. Kwa hiyo kamati ya afya na mpango ya China ikishirikiana na wizara ya elimu zimetoa agizo la kutaka kuanzisha utaratibu wa shule kuripoti hali ya ukimwi, na kuimarisha huduma za upimaji wa ukimwi kwa hiari.
    • Wanawake wasio na waume wapigwa marufuku kugandisha mayai yao ya uzazi
    Tungependa kuwafahamisha wasikilizaji wetu kuwa hapa China wanawake wasio na waume hawaruhusiwi kabisa kuhifadhi au kugandisha mayai yao, ambayo wataweza kuyatumia baadaye wanapohitaji kufanya hivyo, na kwa sasa hapa hapa nchini China suala hili limekuwa likijadiliwa sana kuwa ni kiini cha suala la haki ya uzazi ya mwanamke asiye na mume. Katika nchi zetu za Afrika hususan Tanzania suala hili la kugandisha au kuhifadhi mayai ya uzazi halitekelezwi sana na wanawake, wengi wao wakishaolewa huwa wanatamani kupata mtoto. Na kwa wale ambao hawako kwenye ndoa huwa hata hawafikirii kabisa kugandisha kwani wengi hujitahidi kupata mume ili apate mtoto kabla umri haujampita.
    • Simama na kueneza upendo: Bibi Chen Xiuhua mwenye kansa aanzisha biashara kuwasaidia wengine
    Katika kipindi cha leo, tutamzungumzia Bi. Chen Xiuhua. "Mimi naitwa Chen Xiuhua, mwaka huu ninatimiza miaka 50, mimi ni mwanamke wa kawaida wa kijijini, nina saratani ya shingo ya uzazi, na iko kwenye hatua ya kati au ya mwisho. Lakini nilibahatika sana, watu wengi walinisaidia. Nilifanya mambo ambayo nilitakiwa kufanya, lakini ninakubaliwa na wote. Familia yangu ilichaguliwa kuwa 'familia 10 bora za Chongqing' na 'familia bora nchini China', na niwakilisha 'familia bora' pekee nchini China, na nilipewa tuzo katika Jumba Kuu la Umma la China."
    • Mikopo ta riba nafuu yawanufaisha wanawake wa vijijini nchini China
    Kipindi cha leo tunaelekea huko Guizhou, kusini magharibi mwa China, ambako baada ya mvua ndogo kunyesha, hali ya hewa mlimani inakuwa baridi kidogo. Sasa Pili, huko Guizhou, kuna msemo usemao "hali ya hewa nzuri haizidi siku tatu, eneo la tambarare halitazidi kilomita 1.5, na Guizhou ikinyesha mvua ni kama katika majira ya baridi".
    • Mtandao wa Internet Enzi mpya kwa wanawake kuanzisha biashara
    Katika kipindi kilichopita, tulikufahamisha machache kuhusu Shamba la Familia ya Zhiqing lililoanzishwa na Bi. Zhang Tian, na jinsi lililovyoweza kukwamua familia hiyokiuchumi, lakini pia kuwa mfano kwa wanakijiji wenzake huko Tongnan, mji wa Chongqing, hapa China.
    • Hadithi za shamba la familia ya Zhang Tian
    Kwa muda wa mwaka mmoja na nusu uliopita, hapa China, kampuni zaidi ya elfu 10 zinaanzishwa kila siku. Na hivyo, wimbi la "kuanzisha biashara na kuwa na uvumbuzi kwa wengi" limekuwa nguvu mpya ya kusukuma mbele maendeleo ya uchumi wa China.
    • Wanawake wa mashinani Kenya wapiga hatua kiuchumi kupitia mikopo ya serikali

    Tarehe 15 Oktoba ikiwa ni siku ya Umoja wa Mataifa ya wanawake wanaoishi mashambani, nimefika hapa kaunti ya Kakamega magharibi mwa Keny ambapo nimekutana na vikundi tofauti vya wanawake, ambavyo vimesaidiwa na mashirika yasiyo ya kiserikali, serikali kuu na serikali ya kaunti hili kuanzisha miradi ya kujikimu kimaisha.

    • Kiwango kikubwa siku hadi siku cha kuvunja ndoa
    Katika kipindi cha leo tutazungumzia suala la ndoa na talaka. Kama utakumbuka Pili, kuna mkongwe mmoja wa muziki aliwahi kuimba kuwa 'Kuolewa ni jambo la sifa', na pale binti anapoolewa au kijana anapooa, wazazi, ndugu, na jamaa wanaona fahari sana kwani ni hatua muhimu katika maisha ya mwanadamu. Familia hutumia miezi kadhaa au hata miaka kuandaa harusi, ili tu iwe ya kufana na kuvutia. Lakini sasa, idadi ya ndoa zinazovunjika inaongezeka kwa kasi duniani.
    • Tule kwa Afya- Juisi za matunda asilia na faida zake mwilini
    Tungependa kuwauliza maswali kadhaa wasikilizaji wetu kabla ya kuendelea na utengenezaji wa juisi, mswali yenyewe ni kwamba je unajua kuwa unaweza kuondoa sumu mwilini, kupunguza mafuta mwilini, kupunguza uzito wa mwili na shinikizo la damu kwa kunywa juisi ya matunda asilia iliyotokana na siki ya apple, limao, mdalasini uliosagwa, asali mbichi pamoja na maji? Juisi yenye mchanganyiko huu wa matunda, mdalasini na asali ni kinywaji asilia chenye faida nyingi kiafya. Kwa hiyo tungewashauri wasikilizaji wetu kujenga afya za mwili wao kwa kunywa juisi yenye mchanganyiko huu mara kwa mara.
    • Nafasi ya mwanamke katika jamii
    Katika kipindi cha Sauti ya Wanawake kinachokujia muda kama huu kupitia Idhaa ya Kiswahili ya Radio China Kimataifa. Katika kipindi hiki tunazungumzia masuala mbalimbali yanayomhusu mwanamke na jamii kwa ujumla, changamoto anazokumbana nazo katika jitihada zake za kujikwamua kimaisha, na pia mafanikio ambayo yamepatikana katika suala zima la usawa wa jinsia.
    • Nafasi ya mwanamke kwenye sekta ya habari Afrika Mashariki
    Katika kipindi cha leo, mwenzangu Caroline Nassoro alipata fursa ya kuwahoji wanahabari kutoka vyombo mbalimbali nchini Tanzania kuhusu nafasi ya mwanamke katika tasnia ya habari. Wanahabari hao Bi. Moza Saleh kutoka Hits FM Zanzibar, Khadija Khalili kutoka gazeti la Tanzania Daima, na Mwasu Sware kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania, TBC, walikuja hapa China kwa ziara fupi ya mafunzo. Na kutokana na kuwa, wanahabari wote waliokuja kwenye ziara hiyo ni wanawake, Carol alitaka kujua kama hiyo ni ishara kuwa, nafasi ya mwanamke kwenye tasnia ya habari imeanza kutambulika.
    • Mwanamke anawezaje kutoa uwiano sawa kwa kazi yake na familia?
    Mfumo dume kwa kiasi fulani bado unatawala katika nchi mbalimbali, hususan zile zinazoendelea, ambapo mwanamke anachukuliwa kama chombo cha starehe, na kazi yake kubwa ni kumhudumia mumewe, watoto, na kusimamia nyumba. Mwenzangu Caroline Nassoro alifanya mahojiano na Jane Munji Maina, meneja wa matangazo ya biashara kwenye kituo cha televisheni cha KTN na Radio Maisha vinavyomilikiwa na kampuni ya Standard Group ya Kenya. Na anaanza kwa kueleza changamoto alizokutana nazo hadi kufikia nafasi aliyo nayo sasa, na jinsi gani anaweza kuwa na uwiano kati ya familia, masomo, na kazi.
    • Mapishi ya Tambi za kukaanga, supageti na makaroni
    Wageni wengi wanaotoka katika nchi za nje waliopo hapa China wanapenda kula chaomian yaani tambi zinazokaangwa kwa mafuta, tambi hizi zinaweza kupikwa kwa namna mbalimbali, mbali na kutiwa zhajiangmian yaani vipande vya nyama zilizokaangwa na kuchanganywa na tianmianjiang, na tambi zilizochemshwa pamoja na nyama ya ng'ombe, tambi zinaweza kukaangwa na kuwa chakula kitamu sana. Kuna aina nyingi za mapishi ya chaomian, unaweza kuchagua yale unayopenda.
    • Smartphone app zatumika kukusanya na kuondoa vijidudu kwenye maziwa ya mama nchini Afrika Kusini
    Sote tunafahamu umuhimu wa kumnyonyesha mtoto mchanga, na kuzingatia ule muda uliopendekezwa wa kunyonyesha. Lakini kuna baadhi ya kina mama kwa sababu moja ama nyingine wanashindwa kunyonyesha watoto wao, labda ni kutokana na maradhi, au wanaweza kuwa na sababu zao binafsi. Kitu kimoja kiko wazi, ni muhimu sana kwa mama kumyonyesha mtoto kwa faida ya mama mwenyewe na pia kwa faida ya mtoto.
    • China kusimamia ubora wa vyakula vya woto wachanga na wenye umri wa chini ya miaka mitatu
    Katika kipindi cha leo tutazungumzia kwa kina kuhusu usalama wa vyakula vya watoto, na tumeamua kuzungumzia hili kwa sababu katika miaka ya hivi karibuni, bidhaa zenye maandiko ya "chakula cha watoto" kama vile biskuti za watoto, soy sauce ya watoto, tambi za watoto na nyingine nyingi zinaonekana hapa na pale, na kupokewa vema na watoto na wazazi wao. Lakini swali ni je? Vyakula hivyo ni salama kwa kiasi gani kwa watoto? Wataalam wamedokeza kuwa, hivi sasa China bado haina kigezo maalum kinachohusu vyakula vya watoto, hivyo watu wanapozingatia lishe bora, pia wanapaswa kula kwa kiasi.
    • Pikipiki za kubebea wagonjwa zapunguza kiwango cha vifo vya mama wajawazito
    Vifo vya uzazi ni moja ya tishio kubwa sana la afya. Kila saa 24, takriban wanawake 800 wanafariki kutokana na matatizo ambayo mara nyingi yanaweza kutibika yanayohusiana na ujauzito na kujifungua. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, asilimia 99 ya vifo vya uzazi vinatokea katika nchi zinazoendelea, hususan zile zilizoko kusini mwa Sahara na Asia Kusini. Ndio maana mashirika mbalimbali ya kimataifa, taasisi za afya za kitaifa, na mamlaka za afya zinaungana pamoja kupambana na vifo vya uzazi katika sehemu zinazoathirika zaidi na matatizo hayo. Katika juhudi hizo za kutafuta ufumbuzi wa tatizo la vifo vya uzazi ambalo pia husababishwa na kuchelewa kufika hospitali kwa wajawazito, njia nyepesi ya usafiri ikagunduliwa.
    • Umoja wa Mataifa waanzisha kampeni ya "Okoa Maisha ya Mtoto" ili kuimarisha usalama barabarani kwa watoto
    Wanawake na watoto mara nyingi wamekuwa wahanga wa majanga mbalimbali ya kimaumbile kama vile machafuko, vita, njaa, na majanga mengine kama hayo. Lakini watoto wanakabiliwa na hatari nyingine kubwa, nayo ni ajali za barabarani. Shirika la Afya Duniani, WHO limesema uhai wa watoto uko mashakani kila uchao kutokana na ajali za barabarani. Shirika hilo limesema, kila siku watoto 500 hufariki dunia ilhali wengine wengi hujeruhiwa kutokana na ajali za barabarani, huku ajali hizo zikiwa chanzo kikubwa cha vifo kwa vijana barubaru hususan wavulana.
    • Vitoweo kula kiafya
    Mwezi uliopita tuliwaelezea upishi wa kitoweo cha "Gongbaojiding" ambapo tuliwapasha faida mbalimbali ya viungo vinavyotumika kwenye kitoweo hicho. Katika kipindi cha leo tutaanza kuzungumzia chakula kingine ambacho ni maarufu sana hapa China kiitwacho Jiaozi. Wasikilizaji wetu wengi sana watakuwa wanaifahamu japo kwa kuisikia kwani ni chakula ambacho tumekuwa tukikielezea sana kwenye sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China.
    • Kipindi maalum cha tatu kuhusu Siku ya Albino ya Kimataifa--Hatma yetu sio ndoto
    Katika vipindi viwili vilivyopita tumezungumzia kadhia, au adha wanazokutana nazo Albino. Tulianzia nchini Tanzania na Kenya, tukazungumzia hali ya Albino hapa China, na katika kipindi cha leo, tunazungumzia "Hatma yetu sio ndoto". Katika miaka kadhaa iliyopita, Albino wengi waliuawa kila mwaka, wengi wao ni watoto ambao hata hawakutimia mwaka mmoja. Baada ya kuuawa, viungo vyao vilikatwa na kuuzwa kwenye masoko haramu, kama nyongeza ya dawa za kienyeji na kwa kujilinda. Viungo hivi vinauzwa bei ghali sana, habari zinasema kuwa, bei ya kiungo cha albino imefika dola za kimarekani zaidi ya elfu 3. Masoko hayo yako sehemu nyingi za Afrika mashariki, watu wengi wanafanya biashara hii ingawa ni ya hatari sana.
    • Kipindi maalum cha pili kuhusu Siku ya Albino ya Kimataifa--Familia maalum katika mji wa kale nchini China
    Wiki iliyopita tulikuletea sehemu ya kwanza ya mfululizo wa vipindi vitatu kuhusu Siku ya Kimataifa ya Albino, na tulizungumzia zaidi changamoto wanazokumbana nazo Albino barani Afrika, hususan nchini Tanzania na Kenya. Leo hii tunaendelea na sehemu ya pili, na kama tulivyowaahidi, tutazungumzia changamoto wanazokutana nazo Albino hapa China. Tulitembelea familia za albino na shirika lisilo la kiserikali linaloitwa "familia ya watoto wa mwezi" katika mji wa kale wa China, Xi'an, tukaelewa hali ya maisha, kazi na masomo yao. Na tunakuletea sehemu ya kwanza ambayo tunaiita "familia maalum katika mji wa kale nchini China".
    SearchYYMMDD  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako