• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • • Adhabu ya viboko kwa watoto
    Kuna jambo moja ambalo bado linajadiliwa katika nchi mbalimbali duniani, nalo ni adhabu ya viboko kwa watoto. Kuna baadhi ya nchi adhabu hiyo imefutwa, lakini kuna sehemu ambazo adhabu hiyo bado inatumika, hususan mashuleni na hata majumbani. Kwa mffano nchini Tanzania, adhabu hiyo ilifutwa mashuleni, lakini kutokana na mtokeo mabaya ya wanafunzi, serikali inafikiria kurudisha adhabu hiyo.
    • Tatizo la wanafunzi kulazimishwa kuacha masomo shuleni kutokana na kupata ujauzito
    Mimba za umri mdogo ambazo zinapelekea wanafunzi kukatisha masomo yao bado ni tatizo kubwa katika bara la Afrika. Matukio ya mimba kwa wanafunzi mbali na kuwakatisha masomo lakini pia yamekuwa yakitishia afya zao. Nchini Afrika Kusini, kuna shule maalum, ambayo wanafunzi wote ni wasichana waja wazito. Lengo la kuanzishwa kwa shule hiyo maalum ni kuwasaidia wasichana waja wazito wasisimamishwe masomo yao, na kutengwa na jamii. Ingawa serikali ya Afrika Kusini imetoa amri kwamba shule yoyote isiwafukuze wanafunzi wasichana wakiwa waja wazito, lakini bado kuna wasichana wengi wanaofukuzwa shule au kuacha masomo kutokana na shinikizo kutoka kwenye jamii, hali ambayo inaleta athari kubwa na mbaya kwa maisha yao ya baadaye.
    • Watoto wa shule nchini Kenya wawaokoa wasichana na ubakaji baada ya kufundishwa kauli "NO MEANS NO"
    Tuliwahi kuzungumzia suala la ubakaji na madhara yake kwa wasichana na wanawake. Kwa kuzingatia hali ya sasa ilivyo na kuongezeka kwa matukio ya ubakaji, serikali ya Kenya imeanzisha kampeni ya "NO MEANS NO" maana yake, HAPANA MAANA YAKE NI HAPANA. Kampeni hii inatoa elimu kwa vijana wa kike na kiume kuhusu kupambana na vitendo viovu katika jamii.
    • Vitoweo kula kiafya
    Karibu msikilizaji kwenye kipindi hiki cha sauti ya wanawake, kumbuka ndani ya kipindi tunapata fursa ya kuangalia mambo mbalimbali kuhusu wanawake na watoto, lakini kuanzia kila Jumatatu ya mwisho wa mwezi tukianzia na mwezi huu wa sita tutakuwa tunawaletea sehemu maalumu ya tule kwa afya.
    • Siku ya Baba Duniani
    Tarehe 8 Machi ni Siku ya Wanawake Duniani, na May 10 ilikuwa ni siku ya Mama. Sasa kina baba bao hawako nyuma, kwani tarehe 21 June ni Siku ya Baba. Kina baba nao wameona wasibaki nyuma bali wenyewe wawe na siku yao inayotambulika rasmi! Katika kipindi cha leo, tutazungumzia siku ya Baba, lakini kwa mtazamo wa tamthilia ya kichina ambayo imepata umaarufu mkubwa sana. Tamthilia hiyo inaitwa, 'Baba, tunaenda wapi?' Katika tamthilia hiyo, wakina baba ambao ni maarufu, wanaenda na watoto wao nje ya mji kwa muda wa siku tatu na kuwahudumia watoto hao peke yao, bila ya mama wa watoto kuwepo. Tamthilia hiyo inachekesha lakini pia kuna sehemu zinazosikitisha.
    • Kipindi maalum cha pili kuhusu Siku ya Albino ya Kimataifa--Familia maalum katika mji wa kale nchini China
    Wiki iliyopita tulikuletea sehemu ya kwanza ya mfululizo wa vipindi vitatu kuhusu Siku ya Kimataifa ya Albino, na tulizungumzia zaidi changamoto wanazokumbana nazo Albino barani Afrika, hususan nchini Tanzania na Kenya. Leo hii tunaendelea na sehemu ya pili, na kama tulivyowaahidi, tutazungumzia changamoto wanazokutana nazo Albino hapa China. Tulitembelea familia za albino na shirika lisilo la kiserikali linaloitwa "familia ya watoto wa mwezi" katika mji wa kale wa China, Xi'an, tukaelewa hali ya maisha, kazi na masomo yao. Na tunakuletea sehemu ya kwanza ambayo tunaiita "familia maalum katika mji wa kale nchini China".
    • Kipindi maalum cha kwanza kuhusu Siku ya Albino ya Kimataifa--Malaika wanaoangukia kwenye Ziwa Kuu
    Siku ya Kimataifa ya Albino itaadhimishwa hivi karibuni, na kwa kuzingatia hilo, tumekuandalia mfululizo wa vipindi vitatu kuhusiana na suala hilo. Albino ni watu wenye ulemavu wa ngozi, wanaogopa mwanga wa jua kwani kutokana na ngozi yao ni rahisi sana kuungua na jua, pia uwezo wao wa kuona ni dhaifu, tofauti na mtu wa kawaida. Watu hawa huitwa "watoto wa mwezi".
    • Juhudi za kupambana na ugonjwa wa fistula
    Kwa lugha ya kitalaamu ugonjwa huu hujulikana kama Peri-anal fistula. Ni tatizo la kuwapo kwa tundu au matundu karibu na njia ya haja kubwa. Tundu hilo huwa na mfereji unaojitokeza katika njia ya haja kubwa kwa ndani na hupitisha choo kikubwa bila ya mgonjwa kujitambua au kufahamu. Tatizo hili linatokea wakati mwanamke anapojifungua na linakuwa katika misuli kati ya uke na kibofu cha mkojo au kati ya uke na njia ya haja kubwa au vyote viwili. Ingawa huwakumba zaidi wanawake lakini badhi ya wakati hata wanaume pia nao huugua.
    • Umuhimu wa kunyonyesha watoto wachanga
    Katika kipindi cha leo tutazungumzia umuhimu wa maziwa ya mama, au unyonyeshaji na manufaa yake kwa mama na mtoto pia. Kuna baadhi ya kina mama huwa hawanyonyeshi watoto wao kwa hofu kuwa matiti yao yatalala au saa 12 jioni. Jambo hili linasikitisha sana kwani kunyonyesha ni njia mojawapo muhimu inayomuunganisha mama na mtoto, sasa kama mtoto hatanyonya, hata ule ukaribu na mama pia hautakuwepo. Kwa miongo kadhaa sasa, manufaa ya kiafya kutokana na unyonyeshaji na mapendekezo ya jambo hilo yameendelea kuongezeka.
    • Shinikizo la mama ni kubwa zaidi au la baba?
    Jana dunia nzima iliadhimisha siku ya mama. Tunafahamu kuwa mama ni kiungo muhimu sana cha familia, na kuonesha thamani yake kumekuwa na misemo mbalimbali inayoashiria kuwa mama ni mtu muhimu zaidi katika familia na hata katika jamii, miongoni mwa misemo hiyo ni nani kama mama, hakuna kama mama, hakuna mtakatifu au mtukufu hapa duniani asiyezaliwa na mama na mingineyo. Tunafahamu kuwa kwa nchi za Afrika mama ndiye anayeibeba familia nzima katika masuala mengi tu ikiwemo kulea watoto, kupika, kusafisha nyumba, kumtimizia mume mahitaji yake n.k. Ingawa katika nchi nyingine za nje ya Afrika wanaume wamekuwa wakisaidia kidogo shughuli hizo za ndani.
    • Kujikinga kwa kutumia Wu Shu
    Mwezi Desemba mwaka 2012 dunia ilizizima kutokana na mwanamke mmoja kubakwa nchini India, ambapo baadae alifariki dunia. Kusema kweli tukio hilo lilihuzunisha wengi sana, sio nchini India pekee, bali nchi mbalimbali duniani, wanawake kwa wanaume waliandamana kupinga vitendo vya ubakaji, lakini kwa bahati mbaya, vitendo hivyo bado vinaendelea hata sasa. Nchini Afrika Kusini, mwanaume mmoja amehukumiwa kifungo cha miaka 1,535 jela kwa makosa mbalimbali ikiwemo kuwabaka wanawake 30 katika kipindi cha miaka mitano. Madhara yanayompata mwanamke alifanyiwa kitendo hicho cha kikatili ni makubwa zaidi kimwili na kisaikolojia, na kuna wanawake wengine huamua kujiua kutokana na aibu pamoja na msongo wa mawazo.
    • Yoga inavyotuliza akili za wanawake wafungwa
    Wengi wetu tunafahamu kuwa mazoezi ni muhimu katika mwili wa binadamu. Katika maisha ya kila siku, kila binaadamu anakula na hiyo ndiyo kawaida ya mzunguko wa maisha. Je tunakumbuka kufanya mazoezi ili kuwa na afya bora, au kutuliza akili zetu jibu linaweza kuwa ndio au hapana na hii pia inategemea na hulka ya maisha ya mtu ya kila siku. Kwa kuwa tunanakula kila siku tunahitaji kukitumia chakula tulichokula kwa kufanya mazoezi ili kuepuka maradhi kama ya moyo, kisukari na kuwa na uzito uliokithiri, huna budi kufanya mazoezi katika maisha yako bila kujali umri na jinsia.
    • Picha za ngono kwenye mitandao jinsi zinavyowaathiri vijana
    Tuna msemo usemao shilingi ina pande mbili, kwa maana ya kwamba katika kila kitu kuna uzuri na ubaya wake. Ni sawa na teknolojia, tunaamini kuwa imeleta mambo mengi mazuri lakini pia imechangia kwa kiasi kikubwa kueneza mambo mabaya ikiwemo picha na video za ngono. Mtandao wa internet sasa umekuwa mwalimu mkubwa wa kufundisha masuala ya kujamiiana kwa vijana wengi. Hili ni tatizo kubwa kwasababu unatoa mtazamo mbaya wa kujamiiana na vilevile mtazamo mbaya wa uhusiano wa binadamu, ambapo kwa kiasi kikubwa unachangia ukatili dhidi ya wanawake na kuhamasisha vitendo vibaya.
    • Maendeleo yaliyopatikana katika mambo ya wanawake nchini China na katika nchi za Afrika Mashariki
    Habari kutoka Mkutano wa kwanza wa Kamati ya 6 ya wafanyakazi wanawake ya Shirikisho kuu la wanawake la CHina zimesema, hadi sasa idadi ya jumla ya wafanyakazi wa kike imefikia milioni 137, kiasi hicho kinachukua asilimia 40 ya idadi ya jumla ya wafanyakazi nchini China. Mbali na hayo, kiwango cha elimu cha wanawake pia kimeinuka kwa udhahiri. Kwa mfano idadi ya wafanyakazi wanawake waliopata elimu ya chuo kikuu inachukua asilimia 51.9 ya idadi ya jumla ya wafanyakazi, kiasi hicho kimeongezeka kwa asilimia 34.6 kuliko miaka mitano iliyopita.
    • Kipindi maalum cha Siku ya Wapendanao
    Katika kipindi cha leo tutazungumzia Siku ya wapendanao yaani Valentine's Day iliyokuwa jumamosi iliyopita. Siku hiyo inaonekana kama ni sikukuu ya vijana, na zawadi kama vile chokoleti na maua ya waridi zinazowakilisha mapenzi zinaonekana kila mahali wakati wa sikukuu hiyo. Watu wengi wanasherehekea sikukuu hiyo kwa namna tofauti. Lakini sikukuu hii chimbuko lake ni nini hasa?
    • Sikukuu ya wanawake
    Leo tutazungumzia matumizi salama ya kondomu. Lakini kabla ya kujadili suala hilo, ikumbukwe tu kwamba jana ilikuwa ni siku ya wanawake duniani, na kama kawaida dunia nzima ilijumuika pamoja kuadhimisha siku hii yenye kauli mbiu "Uwezeshaji Wanawake:Tekeleza Wakati ni Sasa".
    • Matumizi yasiofaa ya dawa yaleta athari mbaya kwa watoto
    Katika kipindi cha leo tutazungumzia matumizi yasiyofaa ya dawa za watoto. Unajua Pili mara nyingi mtoto anaweza kukwambia kichwa kinauma, basi unachukua panadol au asprin, unakata nusu au robo, kisha unampa. Binafsi unaona hakuna madhara yoyote, lakini kumbe sivyo. Wataalam nchini China wana hofu kuhusu matumizi yasiofaa ya dawa kwa watoto, na wanashauri wazazi kupata usaidizi wa madaktari ili kulinda watoto kutokana na hatari yoyote.
    • Ukatili dhidi ya wanawake na watoto majumbani
    Ukatili majumbani umeendelea kuwa tatizo kubwa ambalo hadi leo halijaweza kutokomezwa moja kwa moja na wanaume wameendelea kuwa vichwa na viongozi wa familia. Mfumo dume unaendelea kushika hatamu na utamu katika katika jamii nyingi duniani. Wanawake wengi wamekuwa wakidhalilishwa kwa kupigwa na kama haitoshi baadhi ya wakati hata watoto nao pia huingia katika mkumbo huo wa kupigwa majumbani.
    • Ukatili dhidi ya wanawake na watoto majumbani
    Vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinafanyika kila mahali duniani. Kule nchini Tanzania hali ya wanawake pia inazidi kuwa mbaya ndani ya nchi hiyo inayosifiwa kuwa ni nchi ya amani. Kwani kuna tukio moja la kusikitisha sana liliwahi kutokea katika kijiji cha Nyantira Tarime Mara. Akielezea mkasa uliomkuba binti yake Mama mzazi wa binti huyo Bibi Rwakatare alisema, binti yake alikatwa mguu na mume wake na sasa ana mguu kibuku, na sababu kuu ya ukatili huo ni kwamba bawana huyo alikuwa na kimada nje na kumuona mke wake wa ndoa kuwa hana maana yoyote hadi kufikia kumpiga na kumkata mguu wake.
    • Mwitikio wa wananchi wa China kuhusu sera ya kuwa na watoto wawili
    Ni mwaka mmoja sasa tangu sera ya kuwaruhusu wanandoa kuwa na mtoto wa pili kama mmoja kati yao ni mtoto wa pekee katika familia ianze kutekelezwa katika mikoa mbalimbali nchini China. Lakini hali halisi ni kuwa, ombi la kuzaa mtoto wa pili halikuongezeka kwa kiasi kikubwa kama wachina walivyotarajia.
    SearchYYMMDD  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako