• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (9 Julai-15 Julai)

    (GMT+08:00) 2016-07-15 17:46:07

    Zaidi ya watu 85 wauwawa Ufaransa baada ya lori kuparamia umati wa watu

    Zaidi ya watu 85 wamefariki katika mji wa Nice kaskazini mwa Ufaransa baada ya lori moja ambalo lilikuwa likiendeshwa kwa kasi kuparamia kwenye umati mkubwa wa watu.

    Watu hao walikuwa wamekusanyika kujionea fataki katika eneo la Promenade des Anglais, kuadhimisha siku ya kitaifa ya Bastille.

    Kwanza kulikuwa na ufyatuaji wa risasi, polisi wanasema, kabla ya lori hilo kuingia kwenye umati wa watu na kuuwa zaidi ya 85 huku wengi wakijeruhiwa.

    Dereva wa lori hilo amepigwa risasi na kuuwawa na ndani ya lori kumepatikana bunduki na Guruneti.

    Rais wa Ufaransa François Hollande ametoa taarifa kufuatia tukio hilo la mjini Nice akisema ni wazi kuwa hilo ni shambulizi la kigaidi, na kwamba hali ya tahadhari itarefushwa kwa miezi mitatu.

    Hollande baadaye alizuru kwenye mji huo wa Nice, baada ya kuandaa mkutano wa dharura.

    Amesema Ufaransa itaongeza zaidi oparesheni zake nchini Iraq na Syria ambako kundi la Islamic State limejikita.

    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako