• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (9 Julai-15 Julai)

    (GMT+08:00) 2016-07-15 17:46:07

    Aliyekuwa waziri wa Afrika Mashariki kutoka Burundi auwawa

    Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Burundi Hafsa Mossi ambaye pia alikuwa waziri ameuwawa mjini Bujumbura.

    Mbunge huyo ameuwawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana katika barabara ya Gihosha, eneo la Nyankoni, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.

    Msemaji wa serikali ya Burundi Bw Philipe Nzobonariba amesema Bibi Mosi aliuawa, muda mfupi baada ya kuondoka nyumbani kwake.

    Mwaka 2005 Bibi Mosi aliteuliwa kuwa msemaji wa Rais wa Burundi, na baadaye kuteuliwa kuwa waziri wa habari na mambo ya Afrika Mashariki, na mwaka 2012 aliteuliwa kuwa mbunge wa bunge la Afrika mashariki.

    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako