Rais Salva Kiir aamuru kusitishwa haraka kwa mapigano
Nchini Sudan Kusini, Rais Salva Kiir amesaini sheria inayoamuru usitishwaji wa uhasama haraka iwezekanavyo ,hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa katika televisheni na Waziri wa Habari, Michael Makuei.
Mapigano kati ya majeshi ya ya serikali na waasi wa zamani yalianza upya katika mji mkuu, Juba, siku tano zilizopita.
Mapigano makali yameendelea kushuhudiwa Jumatatu hii katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, kati ya vikosi vinavyomtii Rais Salva Kiir na vile vinavyomuunga mkono Makamu wa kwanza wa rais Riek Machar.
Ndege za kivita na vifaru vimeonekana vikitumiwa katika mapigano hayo. Hali hii imesababisha usalama kudorora katika taifa hili changa duniani, na kutishia kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |