• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (9 Julai-15 Julai)

    (GMT+08:00) 2016-07-15 17:46:07

    Theresa May ndiye waziri mkuu wa Uingereza

    Bi Theresa May amechukua usukani kama waziri mkuu wa Uingereza, na mara moja kumchagua Boris Johnson aliyeongoza kampeni ya kuondoka kwa umoja wa Ulaya kuwa waziri wa mambo ya kigeni.

    Akizungumza baada ya kupokea ufunguo wa makao rasmi ya waziri mkuu wa Uingereza 10 Downing Street bi May amehakikishia washirika wake na mataifa ya muungano wa ulaya kuwa licha ya taifa hilo kuamua kujiondoa,

    Uingereza inapania kujiunga na mataifa shirika na kutekeleza wajibu wake katika muungano wa mataifa huru duniani.

    Amesema kuwa serikali yake haitanaswa na mtego wa kuwasikiza mabwenyenye walio wachache na kusahau wananchi wa kawaida.

    May amesema kuwa serikali yake itahakikisha inawakilisha matarajio ya kila muingereza.

    Yeye ndiye mwanamke wa kwanza kuhudumu kama waziri mkuu tangu Margaret Thatcher.

    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako