• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (9 Julai-15 Julai)

    (GMT+08:00) 2016-07-15 17:46:07

    Serikali ya Tanzania yafuta usajili wa magazeti 473

    Serikali ya Tanzania wiki hii imesema imefuta usajili wa karibu nusu ya magazeti nchini humo baada ya wamiliki wa magazeti hayo kushinda kutoka nakala kwa miaka mitatu mfululizo.

    Waziri wa habari wa Tanzania Bw Nape Nnauye amesema uamuzi huo umechukuliwa dhidi ya magazeti 473 kati ya magazeti 881 nchini humo baada ya wamiliki kushindwa kufuata taratibu na kanuni za usajili hata baada ya kuarifiwa kupitia gazette la serikali.

    Bw Nnauye amesema tangazo la kwanza la serikali lilitolewa mwaka 2013 wakati magazeti 550 yalikuwa hayachapishwi. Baada ya tangazo hilo ni magazeti 77 tu yalianza kuchapishwa.

    Waziri Nnauye amesema yeyote atakayechapisha gazeti ambalo usajili wake umefutwa atakabiliwa na hatua za kisheria.

    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako