• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (9 Julai-15 Julai)

    (GMT+08:00) 2016-07-15 17:46:07

    Uganda yapeleka Jeshi Susan Kusini

    Msafara wa wanajeshi wa Uganda waliojihami umeingia Sudan Kusini kufuatia amri ya rais Yoweri Museveni kwenda kuwanusuru waganda walioathirika katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe juma lililopita.

    Msafara huo wa malori 50 ya kijeshi yanapewa usalama na vifaru vidogo vya jeshi la UPDF.

    Msafara huo uliingia ardhi ya Sudan Kusini kupitia kivuko cha Nimule takriban kilomita 200 kutoka Juba na unatarajiwa kuelekea hadi mji huo mkuu kuwanusuru waganda walioko huko.

    Brigadier Leopold Kyanda anasema kuwa hawatutasita kuwasaidia wale wanaotaka kuondoka awe ni Mganda ama hata raia wa Sudan Kusini yenyewe.

    Msemaji wa jeshi Paddy Ankunda amenukuliwa akithibitisha kuwa kikosi kidogo cha wanajeshi kitakwenda kwa barabara kuwaokoa waganda walioathirika na mapigano

    Hatua hiyo ilifuatia ripoti ya mauaji ya wafanya biashara watano raia wa Uganda miongoni mwa watu zaidi ya 272 waliouawa majeshi watiifu kwa rais Salva Kiir walipokabiliana vikali na wanajeshi watiifu kwa makamu wa rais wa Sudan Kusini bw Riek Machar mjini Juba.

    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako