• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( Agusti 20-Agusti 26)

  (GMT+08:00) 2016-08-26 17:56:16
  Raia kuondoka mji wa Daraya Syria

  Makubaliano yamefikiwa wiki hii kuwataka raia na waasi waliopo katika eneo la mapigano katika mji wa Daraya baada ya kuzingirwa kwa muda mrefu na vikosi vya serikali ya Syria .

  Serikali na mmoja wa makamanda wa makundi ya wapiganaji wamekubaliana kuwa raia na askari wa majeshi ya makundi hayo wanapaswa kuondoka leo eneo hilo .

  Vyombo vya habari nchini Syria vimearifu kuwa raia elfu nne na wapiganaji mia saba wataruhisiwa kuondoka eneo hilo.

  Mji wa Daraya ulio karibu na Damascus tangu mwaka 2012 umezingirwa na vikosi vya serikali na kushuhudia mfululizo wa mashambulizi.

  Wakati huo huo mapigano makali yameendelea katika mji wa Aleppo nchini humo pamoja na kuwepo mkazo wa umoja wa mataifa kusitisha mapigano hayo kwa saa 48

  Vikosi vya serikali vinadaiwa kuwaua raia 15 kati yao 11 wakiwa ni watoto kufuatia shambulizi dhidi ya waasi karibu na eneo hilo.

  1 2 3 4 5 6 7 8 9
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako