• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( Agusti 20-Agusti 26)

    (GMT+08:00) 2016-08-26 17:56:16

    Marekani yapokea ombi rasmi la Uturuki la kumrejesha nyumbani shehe Gulen

    Wizara ya mambo ya ndani ya Marekani imesema imepokea ombi rasmi kutoka Uturuki la kumrejesha shehe Fethullah Gulen anayeishi nchini humo.

    Shehe huyo alilaumiwa awali na serikali ya Uturuki kwa kuhusika na jaribio la mapinduzi lililotokewa mwezi uliopita nchini Uturuki.

    Hata hivyo, msemaji wa wizara hiyo Bw. Mark Toner amesema, ombi hilo halina uhusiano na jaribio hilo la mapinduzi, bali ni sababu zingine ambazo zinaifanya Uturuki kutaka shehe huyo arudishwe nchini humo, na kwamba Marekani itatoa uamuzi juu ya suala hilo baada ya kufanya thathmini kamili kuhusu ombi hilo.

    Waziri wa mambo ya sheria wa Uturuki Bw. Bekir Bozdag ameonya kuwa uhusiano wa nchi hizo mbili utaathirika vibaya kama Gulen hatarejeshwa nchini Uturuki, lakini Marekani imesema shehe huyo atarejeshwa kwa kufuata taratibu husika za kisheria.

    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako