• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( Agusti 20-Agusti 26)

    (GMT+08:00) 2016-08-26 17:56:16

    Shughuli za rejea kama kawaida Harare

    Shughuli zimerejea kwenye hali ya kawaida jijini Harare, Zimbabwe baada ya, kushuhudia maandamano Jumatano ya vijana wa upinzani waliokuwa wanapinga unyanyasaji unaofanywa na jeshi la Polisi nchini humo.

    Polisi kwa mara nyingine walitumia mabomu ya machozi na risasi za mpira kuwatawanya maelfu ya vijana wa chama kikuu cha upinzani nchini hujmo cha MDC, waliokuwa wakiandamana kwenda wizara ya mambo ya ndani kuwasilisha malalamiko yao.

    Vurugu zilitokea baada ya Polisi kuikngilia kati maandamano ya vijana hao, ambao walikuwa na mabango yaliyokuwa yanakashifu nguvu kubwa inayotumiwa na Polisi dhidi ya raia.

    Baada ya kuzuiwa na Polisi na kuanza kurushiwa vitoa machozi, waandamanaji waligeuza maandamano yao kuwa uwanja wa vita na kuanza kukabiliana kwa mawe na kikosi cha Polisi wa kutuliza ghasia.

    Jeshi la Polisi nchini Zimbabwe hivi karibuni limejikuta kwenye shinikizo kubwa na kukosolewa kwa sehemu kubwa na makundi mbalimbali ya watetezi wa haki za binadamu wanaodai kuwa limekuwa likitumia nguvu kubwa kuwakabili waandamanaji.

    Upinzani nchini humo unakosoa Serikali ya Rais Mugabe, ambaye wanamtuhumu kwa kuiendesha nchik yao kiimla, huku akidharau maoni ya wananchi na wanasiasa kuhusu namna ya kuinusuru nchik hiyo na hali mbaya ya kiuchumi.

    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako