• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( Agusti 20-Agusti 26)

    (GMT+08:00) 2016-08-26 17:56:16

    Mapogano ya miaka 50 yasitishwa Colombia

    Siku mbili baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya amani baina ya waasi na serikali juu ya mgogoro uliodumu kwa takribani miaka 50 nchini Colombia, Rais wa nchi hiyo Juan Manuel Santos ametoa amri kwa jeshi kusimamisha mapigano dhidi ya kundi la waasi la Farc.

    Rais Santos amesema mapigano yatasitishwa kuanzia usiku wa jumatatu na Farc walitangaza kusitisha mashambulizi mwaka mmoja uliopita.

    Hata hivyo mbali na uamuzi wa serikali ya Colombia kusitisha mashambulizi dhidi ya waasi lakini imekataa kutoa taarifa rasmi za kijeshi mpaka makubaliano yatakapo kamilika.

    Mkataba wa makubaliano ya amani bado unasubiri kupitishwa na wananchi wa Colombia kwa kura yha maoni.

    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako