• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( Agusti 20-Agusti 26)

    (GMT+08:00) 2016-08-26 17:56:16

    Jeshi la Nigeria latangaza kumjeruhi kiongozi wa Boko Haram

    Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa kiongozi wa Boko Haram amejeruhiwa vibaya.

    Abubakar Shekau inaaminika kuwa amelengwa na mashambulizi ambayo yamesababisha vifo vingi na jeshi la Nigeria limeeleza kuwa mashambulizi hayo ya anga ni ya aina yake.

    Jeshi la Nigeria limetangaza Jumanne kwenye akaunti yake ya Twitter kwamba maafisa wengi wa kundi la Boko Haram wameuawa katika mashambulizi ya anga na kiongozi wa kundi la kigaidi, Abubakar Shekau, amejeruhiwa vikali.

    Jeshi la Nigeria linasema kuwa mashambulizi hayo yalifanyika Ijumaa ya wiki iliyopita wakati wa sala katika kijiji cha jimbo la Borno, karibu na msitu maarufu wa Sambisa unaotumiwa na kundi la Boko Haram kama ngome yao kuu.

    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako