Watu 5000 kuondolewa katika mji wa Daraya uliozingirwa nchini Syria
Watu elfu 5, wakiwemo waasi wenye silaha, wanatarajiwa kuondolewa kwenye mji uliozingirwa wa Daraya ulioko magharibi mwa mji mkuu wa Syria, Damascus, baada ya makubaliano kufikiwa hivi karibuni kati ya vikosi vya upinzani na jeshi la serikali ya Syria.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo, raia zaidi ya 4000 watahamishwa kwenye makazi ya muda yaliyoko mjini Damascus, huku wapianaji 700 watasalimisha silaha zao na kupelekwa mkoa wa Idlib ulioko kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
Raia na waasi wanaotaka kubaki mjini humo, watapata msaada wa kibinadamu na huduma za matibabu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |