• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( Agusti 20-Agusti 26)

    (GMT+08:00) 2016-08-26 17:56:16

    Watu 250 wafariki baada ya tetemeko la ardhi Italia

    Idadi ya watu waliofariki kwenye tetemeko la ardhi lililotokea nchini Italia Jumatano hii imeongezeka na kufikia watu 250.

    Tetemeko hilo linalokadiriwa kuwa na nguvu ya 6.2 katika vipimo vya Ritcher limesababisha madhara makubwa kwenye miji ya Umbria, Amatrice, Accumoli na Pescara del Tronto kwa watu kufukiwa kwenye vifusi.

    Maeneo yaliyokumbwa zaidi na uharibifu huo ni Accumoli na Pescara del Tronto huku tetemeko hilo likitajwa kuanzia kwenye Norcia, kilomita 170 kaskazini magharibi mwa mji mkuu Roma.

    Shughuli za uokoaji bado zinaendelea.

    Na kwingineko tetemeko la ardhi la kiwango cha Richter 6.5 lilitokea nchini Myanmar na kuuwa watu 3; mtikisiko umesikika katika nchi jirani za Thailand, Bangladesh na India

    Lilikuwa na kina cha kilomita 84 kulingana na idara ya jiolojia ya Marekani na lilitokea kilomita 25 hivi magharibi mwa Chauk.

    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako