• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • China na Marekani zahimiza utatuzi wa mvutano wa kibiashara

  • Pendekezo la China lachangia ujenzi wa mustakabali wa pamoja katika mtandao wa Internet
  Mkutano wa sita wa Mtandao wa Internet duniani umefunguliwa leo mjini Wuzhen, mkoani Zhejiang, China.
  Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi ambayo ilichambua kwa kina mustakabali wa maendeleo ya mtandao wa Internet, na kudhihirisha kuwa ni jukumu la pamoja kwa jumuiya ya kimataifa kuendeleza, kutumia na kusimamia vizuri mtandao wa Internet ili kuufanya uhudumie vizuri binadamu.
  • Uchumi wa China waendelea kwa utulivu ingawa unakabiliwa na changamoto

  Takwimu zilizotolewa leo na Idara Kuu ya Takwimu ya China zinaonesha kuwa, katika robo tatu za mwanzo mwaka huu, pato la taifa la China GDP limezidi dola za kimarekani trilioni 9.87, na kuongezeka kwa asilimia 6.2 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hiki.

  • China yaonesha imani ya kiuchumi kwa kufungua zaidi sekta ya fedha

  Serikali ya China imeamua kurekebisha sheria kuhusu usimamizi wake kwa makampuni ya nje ya bima na benki, ili kufungua mlango zaidi kwa sekta ya fedha, hatua inayoonesha imani ya China kuhusu uchumi wake, na pia italeta injini mpya kwa ukuaji wa uchumi wa dunia.

  • Marekani kujidhuru kimaslahi kwa kuingilia mambo ya Hong Kong

  Baraza la chini la bunge la Marekani jana lilipitisha "Mswada wa sheria wa mwaka 2019 kuhusu haki za binadamu na demokrasia ya Hong Kong", likiunga mkono watu wenye msimamo mkali na wanaofanya vurugu mkoani Hong Kong, China. Kitendo hicho si kama tu kimekiuka sheria za kimataifa na kuingilia mambo ya ndani ya China, bali pia kitadhuru maslahi ya Marekani.

  • China na Marekani zasuluhisha mvutano wa kibiashara kwa njia mwafaka

  Duru mpya ya mazungumzo ya ngazi ya juu kati ya China na Marekani kuhusu suala la kibiashara imefanyika hivi karibuni mjini Washington, na kupiga hatua halisi katika sekta mbalimbali zikiwemo kilimo, ulinzi wa hakimiliki za kiubunifu, kiwango cha ubadilishaji wa fedha, huduma za kifedha, kupanua ushirikiano wa kibiashara, utoaji wa teknolojia, na utatuzi wa migongano. Pande hizo mbili zitaendelea na mazungumzo hayo ili kufikia makubaliano ya mwisho.

  • China siku zote inalinda usalama wa chakula duniani
  • Kuendeleza biashara za huduma kunahitaji kuimarisha ushirikiano wa kimataifa
  • Ongezeko la hatari ya uchumi wa dunia lahitaji kuimarisha utaratibu wa dunia yenye ncha nyingi
  • China yadumisha uwezo mkubwa wa ushindani duniani
  Ripoti kuhusu uwezo wa ushindani duniani ya mwaka 2019 iliyotolewa leo kwenye Baraza la Uchumi Duniani huko Geneva, Uswis, imeonesha kuwa, China inashika nafasi 28 kutokana na uwezo wa ushindani.
  • China yatoa onyo kwa kamishina wa NBA kutochanganya "kauli inayoharibu mamlaka ya nchi" na "uhuru wa kutoa maoni"
  Hivi karibuni mkuu wa Timu ya The Houston Rockets ya Marekani Daryl Morey alitoa kauli ya kuunga mkono waandamanaji katika mkoa wa Hongkong na kukataa kuomba radhi. Naye kamishina wa Ligi ya Mpira wa Kikapu Adam Silver alitangaza hadharani kuunga mkono haki ya Morey ya kutoa maoni yake kwa uhuru. Tarehe 8 Oktoba, chaneli ya michezo ya Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG lilitoa taarifa kwa mara nyingine tena kusimamisha mpango wa kutangaza michezo ya NBA. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China ameeleza bayana kwamba, haistahili kufanya mawasiliano na ushirikiano na China bila ya kuelewa maoni ya watu wa China.
  • China yatoa uzoefu mzuri kwa juhudi za kupunguza umaskini duniani

  Zaidi ya Wachina milioni 850 wameondolewa kwenye umaskini uliokithiri katika miongo saba iliyopita tangu kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, na kati ya mwaka 2013 hadi 2018, kila mwaka zaidi ya watu milioni 12 waliondokana na umaskini nchini China. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri yenye kichwa cha "China yatoa uzoefu mzuri kwa juhudi za kupunguza umaskini duniani".

  • Moyo wa mshikamano na kufanya kazi kwa bidii ni chanzo cha "Muujiza wa China"

  China imefanya maadhimisho makubwa ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China. Kama rais Xi Jinping wa China alivyosema wakati akihutubia katika maadhimisho hayo, mshikamano ni uhakikisho muhimu wa China na wananchi wake kushinda changamoto na kupata mafanikio moja baada ya mengine. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri yenye kichwa cha "Moyo wa mshikamano na kufanya kazi kwa bidii ni chanzo cha "Muujiza wa China".

  • Kujiendeleza kwa amani ni ahadi thabiti ya China kwa dunia

  Maadhimisho makubwa ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China yamefanyika leo kwenye Uwanja wa Tian'anmen mjini Beijing. Rais Xi Jinping amehutubia maadhimisho hayo akisema, China itaendelea kushirikiana na nchi nyingine duniani kusukuma mbele ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja. Shirika kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri yenye kichwa cha "Kujiendeleza kwa amani ni ahadi thabiti ya China kwa dunia nzima"

  • China inayojiendeleza kwa amani siku zote inatuliza maendeleo ya dunia

  Serikali ya China hivi karibuni imetoa waraka wenye jina "China na dunia katika zama mpya", na kufafanua kuwa katika miaka 70 iliyopita, wakati China ilipojiendeleza kwa kujitegemea na kufanya kazi kwa bidii, imeleta manufaa makubwa kwa amani na maendeleo ya dunia. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri ya "China inayojiendeleza kwa njia ya amani siku zote yatuliza maendeleo ya dunia".

  • Marekani kuingilia mambo ya ndani ya Hongkong kunaharibu maslahi ya nchi nyingine na kujidhuru yenyewe
  • Uwekezaji katika soko la hisa la A la China wavutia zaidi uwekezaji wa kimataifa
  Uamuzi wa kipimo cha Dow Jones wa kulihusisha soko la China la ngazi A kwenye kiashiria chake umeanza rasmi leo, hali inayoonesha kuwa, mvuto wa soko la hisa la China na uchumi wa China umekuwa ukiongezeka.
  • Uvumbuzi waleta injini mpya kwa maendeleo ya uchumi wa China

  Benki ya Dunia, kituo cha utafiti wa maendeleo cha baraza la serikali la China na wizara ya fedha ya China leo wametoa ripoti ya pamoja ya "China yenye uvumbuzi, injini mpya ya maendeleo ya uchumi wa China", ikionesha kuwa uchumi wa China unabadilika na kuingia katika hali mpya ya kawaida, na uchumi mpya unaibuka kwa haraka kufuatia ongezeko la uwezo wa uvumbuzi. Radio China Kimataifa imetoa tahariri kuhusu ripoti hiyo.

  • China na Marekani zaweka mazingira ya kusaidia mazungumzo kwa moyo wa dhati na vitendo halisi
  • China yaendelea kuvutia mitaji ya kigeni
  Maonesho ya biashara na uwekezaji wa kimataifa ya Xiamen mwaka huu yaendelea huko Xiamen, kusini mwa China, na mitaji ya kigeni inayotumiwa katika mikataba iliyosainiwa katika maonesho ya biashara ya mazao ya kilimo ya "Ukanda Mmoja na Njia Moja" imefikia dola bilioni 2.95 za kimarekani. Wakati huohuo, Shirika la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa limetoa rasmi "Ripoti ya Uwekezaji wa Dunia 2019" ikionesha kuwa katika mustakabali ambao uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni duniani unapungua kwa miaka mitatu, uwekezaji wa kigeni unaovutiwa na China unaendelea kuongezeka. Hali hii imethibitisha tena kuwa China ni nchi inayovutia uwekezaji mwingi zaidi duniani.
  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 next
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako