• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Marekani haina haki ya kutetea uhuru wa kutoa maoni kwa vitendo vyake vya kuwatendea vibaya wanahabari

  Maandamano makubwa kutokana na kuuawa kwa Mmarekani mweusi George Floyd na polisi mzungu yanaendelea nchini Marekani, huku wanahabari wengi wanaoripoti maandamano hayo wakitendewa vibaya na polisi. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri ikisema, Marekani haina haki ya kutetea uhuru wa kutoa maoni kutokana na vitendo vyake vya kimabavu dhidi ya wanahabari.

  • Waziri wa mambo ya nje wa Marekani ni tishio kweli kwa nchi za Ulaya

  Ingawa Marekani inakabiliwa na maambukizi ya virusi vya Corona na maandamano dhidi ya ubaguzi wa rangi, lakini waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Mike Pompeo ambaye ni "waziri mbaya zaidi wa mambo ya nje wa Marekani katika historia" bado hajaacha kutoa kauli zisizo na msingi, akisema China inaharibu maslahi ya Marekani na wenzake wa Ulaya, ambao wanapaswa kushirikiana kupinga China. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri ikisema, Pompeo ni tishio kwa nchi za Ulaya.

  • Marekani yachukua vigezo tofauti kwa maandamano yanayotokea nchini humo na mkoani Hong Kong

  Hivi karibuni mwanaume Mmarekani mwenye asili ya Afrika wa jimbo la Minnesota, Marekani, aliuawa na polisi wazungu, na tukio hili limesababisha maandamano makubwa katika miji zaidi ya 70 nchini humo. Serikali ya Marekani imedai maandamano hayo ni vurugu, na waandamanaji wanaopinga ubaguzi wa rangi ni wahalifu, na kuwasifu polisi waliogonga waandamanaji kwa gari na kusema ni mfano wa kuigwa. Pia imetishia kutuma majeshi na kuwafyatua risasi za moto waandamanaji. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri, ikisema Marekani imechukua vigezo tofauti kwa maandamano yanayotokea nchini humo na mkoani Hong Kong.

  • Kudumisha utulivu wa uchumi wa China kusukuma mbele uchumi wa dunia

  Mkutano wa Bunge la Umma la China ulifungwa jana hapa Beijing. Kwenye mkutano na wanahabari baada ya kufungwa, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amefafanua masuala mbalimbali yakiwemo maendeleo ya uchumi wa China, kufungua mlango na ushirikiano, na kuonesha nia thabiti ya China katika kutimiza malengo ya maendeleo ya mwaka huu, kuboresha maisha ya watu na kuchangia maendeleo ya uchumi wa dunia.

  • Rais Xi asisitiza kutoa kipaumbele cha wananchi
  • China ina uwezo wa kutimiza malengo ya maendeleo

  Ripoti ya kazi za serikali inayotolewa kila mwaka kwenye mkutano wa Bunge la Umma la China ni kiashiria muhimu cha mwelekeo wa maendeleo ya uchumi na utungaji wa sera. Ripoti ya mwaka huu haikutaja lengo la ukuaji wa uchumi, na imesisitiza kuhakikisha ajira na maisha ya watu, kushinda vita dhidi ya umaskini, na kujitahidi kumaliza ujenzi wa jamii yenye maisha bora kwa pande zote.

  • Waziri wa mambo ya nje wa Marekani anavuruga uhusiano kati ya China na Marekani

  Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alitoa salamu za kumpongeza Tsai Ing-wen kwa kuapishwa kuwa kiongozi wa Taiwan, akimwita rais wa Taiwan, na kusema uhusiano kati ya Marekani na Taiwan ni wa kiwenzi. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri ikisema, Pompeo amekuwa kirusi cha kisiasa kinachovuruga uhusiano kati ya Marekani na China.

  • China ina uwezo wa kutimiza lengo la kutokomeza umaskini unaokithiri mwaka huu

  Mikutano miwili mikuu ya kisiasa nchini China ni majukwaa ya kutoa ishara za sera, na pia ni dirisha linalotumiwa na jamii ya kimataifa kutazama nchi hiyo. Katika mikutano hiyo ya mwaka huu, pande nyingi zinafuatilia jinsi China itakavyotimiza malengo ya maendeleo ya uchumi na jamii, haswa lengo la kutokomeza umaskini uliokithiri.

  • Wanasiasa wa Marekani wanataka kuwa bingwa wa kukwepa wajibu?

  Rais Donald Trump wa Marekani hivi karibuni kwenye mtandao wa kijamii ameweka barua aliyomwandikia mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Tedros Ghebreyesus, akitishia kwamba, kama shirika hilo halitafanya mageuzi makubwa ndani ya siku 30, Marekani haitalifadhili tena, na kufikiria kujitoa kwenye shirika hilo. Kuhusu kauli hiyo, Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri ikiuliza, je, wanasiasa wa Marekani wanataka kuwa bingwa wa kukwepa wajibu.

  • Uchumi wa China wafufuka baada ya mlipuko wa COVID-19

  Mikutano Mikuu Miwili ya kisiasa nchini China itafanyika kuanzia kesho, wakati dunia inakabiliwa na kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona na kudidimia kwa uchumi, jamii ya kimataifa inafuatilia sana jinsi China itakavyohimiza maendeleo ya uchumi wakati wa kukabiliana na virusi hivyo. Shirka Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri, ikisema China ina imani na uwezo wa kushinda changamoto, na kutimiza malengo ya maendeleo ya uchumi na jamii.

  • Baadhi ya wanasiasa wa Marekani hawatafanikiwa katika suala la Taiwan kujiunga na mkutano wa afya wa dunia

  • Rais wa Marekani apuuza sayansi katika michezo yake ya kisiasa

  Kampeni ya urais ya Donald Trump ya mwaka 2016 ilivutia vyama vingi kutokana na chuki yake ya wazi dhidi ya sayansi, ikiwemo nadhari ya kuwa na mashaka juu ya chanjo, na madai yake kuwa mabadiliko ya hali ya hewa ni mzaha ulioanzishwa na China.

  • China yaimarisha imani ya jumuiya ya kimataifa katika kukabiliana na COVID-19

  Rais Xi Jinping wa China jana alipohutubia ufunguzi wa mkutano wa 73 wa Afya wa Dunia, alijulisha uzoefu wa China katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona, kutoa mapendekezo sita ya kuimarisha juhudi za kupambana na virusi hivyo, na kutangaza hatua tano za kusukuma mbele ushirikiano wa kimataifa. Hotuba hiyo itaimarisha imani ya dunia kushinda virusi hivyo, na kukamilisha mfumo wa usimamizi wa mambo ya kimataifa.

  • Wanasiasa wa Marekani wafanya ubaguzi wa rangi wakati wa janga la COVID-19

  • Marekani yafanya umwamba katika chanjo dhidi ya COVID-19

  Zaidi ya viongozi 140 wa nchi mbalimbali wakiwemo rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, waziri mkuu wa Pakistan Bw. Imran Khan na waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Gordon Brown wameandika barua ya pamoja, wakitaka nchi zote zipate chanjo dhidi ya virusi vya Corona kwa usawa, kama ikitafitiwa na kutengenezwa kwa mafanikio.

  • Viongozi wa Marekani wapaswa kuwajibika na kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona duniani
  Hivi karibuni, msomi maarufu wa Marekani Bw. Noam Chomsky ameilaani serikali ya nchi hiyo akieleza kuwa ili kuficha makosa waliyoyafanya kwa Wamarekani, viongozi wa Marekani wametafuta njia ya kuhamisha uwajibikaji wao.
  • Marekani yachukulia mapambano dhidi ya COVID-19 kama ni michezo ya kisiasa

  Gazeti la The Sydney Morning Herald la Australia limetoa ripoti likisema, waraka wenye kurasa 15 uliotolewa tarehe 2 na Gazeti la The Daily Telegraph na kudai chanzo cha virusi vya Corona ni Maabara ya Utafiti wa Virusi ya Wuhan, China, unatokana na habari mbalimbali zisizo sahihi, na kuaminiwa kuwa umetolewa na mwanadiplomasia wa Marekani nchini Australia. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri, na kusema Marekani inachukulia mapambano dhidi ya COVID-19 kama ni michezo ya kisiasa.

  • Wanasiasa wa Marekani wanawachukua wananchi kama chombo cha kufanyiwa majaribio

  Mkurugenzi wa zamani wa Idara ya utafiti na maendeleo ya matibabu ya kiikolojia ya Marekani Bw. Rick Bright ameilaani serikali ya Marekani kwa kulazimishwa kutii amri mbele ya mambo ya kisiasa na kuacha kufuata mapendekezo ya wataalamu hodari wa sayansi kwenye serikali wakati inapotoa maamuzi kuhusu mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

  • Mashambulizi yanayofanywa na baadhi ya wanasiasa wa Marekani yatawaharibia wenyewe

  Wakati hali ya maambukizi ya virusi vya Corona ikionesha mwelekeo mzuri huku maisha ya kawaida ya watu yakirejea hatua kwa hatua katika nchi nyingi duniani, Marekani ikiwa nchi pekee inayoongoza duniani inadumisha ongezeko la idadi ya watu walioambukizwa zaidi ya elfu 20 kwa siku, hali ambayo inasikitisha watu.

  • Sekta ya utalii stawi yaonesha kufufuka kwa uchumi wa China

  Takwimu zilizotolewa na Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China zinaonesha kuwa, katika siku tano za mapumziko ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Wachina zaidi ya milioni 115 walifanya utalii. Hali hii inaonesha kuwa athari ya mlipuko wa virusi vya Corona ni ya muda mfupi, na uchumi wa China unafufuka kwa haraka.

  1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako