• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Marekani yaendelea kuingilia kati mambo ya Mashariki ya Kati
  • China yajiunga na kigezo cha ujumla cha Barclays cha Bloomberg
  • China na Marekani zinatarajiwa kubeba kwa pamoja wajibu kwa dunia

  Siku ya Alhamisi rais Donald Trump wa Marekani alipokutana na naibu waziri mkuu wa China Bw. Liu He, aliyeongoza ujumbe wa China katika mazungumzo ya kibiashara ya duru la 9 kati ya China na Marekani, alisema anapenda kuona pande mbili zinafikia makubaliano ya kihistoria ya pande zote mapema iwezekanavyo, hali ambayo si kama tu itazinufaisha Marekani na China, bali pia dunia nzima. Vile vile alipojibu swali la mwandishi wa habari wa Shirika la vyombo vya habari la China CMG. Rais Trump alisema Marekani na China zina wajibu kwa dunia.

  • Hainan yashuhudia tena China kuzidi kufungua mlango wake
  Katika mkutano wa baraza la Boao la Asia uliofanyika mwaka jana mkoani Hainan, rais Xi Jinping wa China alitangaza kuzidi kulegeza masharti ya soko, kujenga mazingira ya uwekezaji yenye mvuto mkubwa zaidi, kuimarisha ulinzi wa hakimiliki ya ujuzi, kuzidi kuongeza manunuzi ya bidhaa kutoka nje, na kuanzisha duru mpya ya ufunguaji mlango zaidi ya China. Baada ya mwaka mmoja, katika mkutano wa mwaka wa baraza hilo, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametoa tena ishara za kufungua mlango zaidi. Hainan ambayo ni dirisha muhimu la sera za ufunguaji mlango na mageuzi katika miaka 40 iliyopita, imeshuhudia tena China kuzidi kufungua mlango wake.
  • China yatoa mapendekezo kwa ufumbuzi wa matatizo makuu yanayokabili usimamizi wa mambo ya dunia

  Sherehe ya kufungwa kwa Baraza la usimamizi wa mambo ya dunia kati ya China na Ufaransa ilifanyika jana huko Paris, rais Xi Jinping wa China alitoa hotuba kuhusu "kuchangia busara na nguvu katika kuijenga dunia iwe nzuri zaidi", akitoa mapendekezo ya China kuhusu ufumbuzi wa matatizo makuu yanayokabili usimamizi wa mambo ya dunia, na kuzitaka nchi mbalimbali kuchukua hatua halisi katika mambo hayo, na kufanya juhudi za pamoja ili kutimiza kujiamulia mustakabali kwa binadamu.

  • China na Ufaransa zina msimamo wa thamani wa pamoja katika maoni ya usimamizi wa ulimwengu
  Ujenzi wa barabara kuu namba 1 inayounganisha Brazzaville, mji mkuu wa Jamhuri ya Kongo na kituo kikuu cha uchumi Pointe-Noire ulikamilika mwaka 2016, na ulipunguza muda wa safari kati ya miji hiyo miwili kutoka wiki moja hadi saa 6. Barabara kuu hiyo ilijengwa na kampuni ya CSCEC ya China na kusimamiwa na kampuni ya EGIS ya Ufaransa. Baada ya kujengwa kwa barabara kuu hiyo, China na Ufaransa zimeshirikiana tena, China ikiwajibika na ukarabati wa uendeshaji wa barabara na Ufaransa ikishughulikia usimamizi wa uendeshaji huo.
  • Kanuni kadhaa zinastahili kufuatwa katika kuendeleza uhusiano kati ya China na Ufaransa
  Rais Xi Jinping wa China amesema China na Ufaransa ni marafiki wasio wa kawaida. Kwani Ufaransa ni nchi ya kwanza ya magharibi iliyoanzisha uhusiano wa kibalozi na Jamhuri ya Watu wa China, na pia ilitangulia katika kuanzisha ushirikiano na China katika mambo mbalimbali, ikiwemo kuanzisha safari za ndege ya moja kwa moja kati yake na China, kujenga kituo cha utamaduni wa kichina, na kuanzisha idara ya lugha ya kichina katika vyuo vikuu.
  • Rais Xi Jinping wa China kuanza ziara nchini Monaco
  Kutokana na mwaliko wa mfalme Albert Alexandre Louis Pierre Grimaldi wa Monaco, rais Xi Jinping wa China leo anatarajiwa kufika Monaco na kuanza ziara rasmi nchini humo, ikiwa ni mara ya kwanza kwa rais wa China kuitembelea nchi hiyo tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi mwaka 1995. Ziara hiyo imetoa ishara wazi duniani kuwa haijalishi kama nchi ni kubwa au ndogo, au ziko umbali wa kiasi gani, zinaweza kuwa wenzi wa ushirikiano wa kunufaishana.
  • China na Italia zatia nguvu mpya kwenye Njia ya Hariri ya Kale
  Rais Xi Jinping wa China Ijumaa alianza ziara rasmi nchini Italia, ambapo alihudhuria sherehe kubwa ya kumkaribisha iliyoandaliwa na mwenyeji wake Bw. Sergio Mattarella na kufanya mazungumzo naye, na kukutana kwa pamoja na wajumbe kutoka sekta za uchumi na utamaduni wa nchi hizo mbili. Pia rais Xi alikutana na spika wa bunge la Italia siku hiyo.
  • Uchumi wa China kudumisha ukuaji imara
  • Ripoti yaonesha kuwa ushawishi wa China duniani umezidi wa Marekani
  • Uingereza yakataa kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano
  • Suala la Brexit huenda litatatuliwa kwa haraka

  Bunge la Uingereza jana lilikata kwa mara nyingine makubaliano ya Brexit yaliyorekebishwa na serikali inayoongozwa na waziri mkuu wan chi hiyo Bi. Theresa May, ikiwa ni mara ya pili kwa bunge hilo kufanya hivyo tangu mwezi Januari mwaka huu.
  • Ukuaji mzuri wa uchumi wa China wawashangaza watu waliokuwa na shaka juu ya uchumi wa China
  Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang alitangaza vipimo 36 muhimu vya uchumi wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Bunge la Umma la China mwaka jana, akiwakilisha baraza la serikali kutoa ripoti ya kazi ya serikali. Hii leo, serikali ya China imetangaza kuwa majukumu hayo yote yametimizwa.
  • Viongozi wa Korea Kaskazini na Marekani wakutana kwa mara ya pili
  Kiongozi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong Un na rais Donald Trumps wa Marekani kwa nyakati tofauti wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na mazungumzo ya kikundi cha ujumbe mjini Hanoi, Vietnam, lakini mazungumzo yamemalizika mapema.
  • Zama ya 5G itakayowadia yahitaji ufunguaji mlango na ushirikiano wa kimataifa
  Hili ni suala linalojadiliwa zaidi kwenye Mkutano wa mawasiliano ya simu duniani unaofanyika mjini Barcelona, Hispania, ni ujio wa zama ya 5G, ambayo ni ishara wazi inayooneshwa kutoka mkutano huo kwa dunia nzima.
  • Jumuiya ya nchi za kiarabu na Umoja wa Ulaya zaimarisha ushirikiano ili kukabiliana na changamoto

  Mkutano wa kwanza wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu na Umoja wa Ualya umefungwa huko Sharm el Sheikh, nchini Misri, na kuhudhuriwa na viongozi zaidi ya 50 kutoka nchi za kiarabu na za Ulaya. Mafanikio yaliyopatikana kwenye mkutano huo yameonesha kuwa taasisi hizo mbili kubwa za kikanda zina makubaliano mengi zaidi ya pamoja kuliko tofauti.

  • China na Marekani zinatakiwa kuendelea kufanya juhudi ili kupanua maslahi yao zaidi

  Duru ya saba ya mazungumzo ya ngazi ya juu ya kibiashara kati ya China na Marekani yalimalizika tarehe 24 Jumapili mjini Washington. Kwenye mazungumzo hayo ya siku nne, pande mbili zimekubaliana kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa nchi mbili walipokutana nchini Argentina, na kupata maendeleo halisi juu ya masuala ya uhamisho wa teknolojia, ulinzi wa haki miliki ya ubunifu, vizuizi visivyo ushuru, sekta za huduma na kilimo, kiwango cha ubadilishanaji wa fedha na mengineyo. Wakati huohuo, rais Donald Trump wa Marekani amesema kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa ataahirisha mpango wa kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China zitakazoingizwa Marekani uliopangwa kuanza tarehe mosi mwezi Machi.

  • China na Marekani zina maslahi ya pamoja katika ulinzi wa hakimiliki za ubunifu

  Mazungumzo ya ngazi ya juu ya kibiashara kati ya China na Marekani yanayoendelea mjini Washington, Marekani yamepiga hatua chanya katika masuala ya uwiano wa biashara, kilimo, utoaji wa teknolojia, ulinzi wa hakimiliki za ubunifu, huduma za kifedha na mengineyo. Kati ya masuala hayo, nchi hizo mbili zimeafikiana zaidi katika ulinzi wa hakimiliki za ubunifu, kwani zina maslahi mengi ya pamoja katika suala hilo.

  • Hatua kubwa yapigwa mbele katika mjadala wa China na Marekani
  Mjadala wa 6 wa ngazi ya juu kuhusu mambo ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani ulimalizika jana hapa Beijing. Kwa mara ya kwanza rais Xi Jinping wa China alikutana na ujumbe wa Marekani tangu hali ya mvutano ianze kupanda ngazi mwezi Februari mwaka jana.
  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako