• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Nchi ipi yakandamiza na kutishia nchi nyingine duniani?

  Hivi karibuni zaidi ya wamarekani 100 wenye uhasama na China wameandika barua ya pamoja kwa rais Donald Trump wa nchi yao, wakishutumu China kwa "kukandamiza na kutishia nchi nyingine kwa kutumia nguvu yake kubwa". Kauli hiyo imeshangaza watu wengi, ambao wanaona kuwa Marekani ni nchi inayokandamiza na kutishia zaidi nchi nyingine.

  • Vitendo vya umwamba vya Marekani vyaharibu utaratibu wa kimataifa

  Hivi karibuni zaidi ya wamarekani 100 wenye uhasama na China wamesaini barua ya pamoja ya kushutumu China kupuuza kanuni na utaratibu wa kimataifa, na kuchochea serikali ya nchi hiyo kupingana na China. Barua hiyo inapotosha ukweli, na kuonesha kuwa watu hao hawana uelewa mzuri wa mambo ya China.

  • Soko la hisa la China lafungua ukurasa mpya

  Soko la hisa la China limefungua ukurasa mpya, baada ya hisa za kwanza za makampuni 25 ya teknolojia na uvumbuzi kuanza kuuzwa kwenye soko hilo leo asubuhi.

  • Wanasiasa wenye hila wa Marekani hawana haki ya kulaani mambo ya kidini nchini China

  Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Michael Pompeo kwa nyakati tofauti wametoa hotuba ya kuipaka matope China katika mambo ya kidini.

  • Ulaya hatakiwi kutoa alama zenye kosa katika suala la Hong Kong

  Bunge la Ulaya jana lilipitisha azimio linalohusiana na Hong Kong, likiitaka serikali ya Hong Kong kuondoa mashtaka dhidi ya waandamanaji waliofanya vurugu bila ya sababu na kuanzisha uchunguzi kuhusu vitendo vya utekelezaji wa sheria vya polisi wa Hong Kong. Azimio hilo limepuuza vitendo vibaya vya kimabavu vilivyotokea hivi karibuni Hong Kong, na limekosa msimamo wa msingi wa utawala wa sheria na pia ni uchokozi mbaya kwa utaratibu wa utawala wa sheria wa Hong Kong na kuingilia siasa za ndani za China. China inalaani vikali na kupinga kithabiti azimio hilo.

  • China kuzidi kulinda hakimiliki za ujuzi katika pande nyingi
  Idara ya hakimiliki za ujuzi ya taifa ya China hivi karibuni imetangaza hakimiliki mpya ya ujuzi ya kampuni ya Huawei, ambayo ni "njia na vifaa vya kielektroniki vya kupiga picha za mwezi". Baada ya hapo, mkutano wa kawaida wa baraza la serikali ya China uliofanyika jana, umeamua kuchukua mfululizo wa hatua ili kuzidi kuimarisha nguvu ya kulinda hakimiliki za ujuzi. Uvumbuzi wa China unaendelea kwa kasi, na ulinzi wa hakimiliki za ujuzi ukiwa nguvu kubwa zaidi ya kuhimiza uvumbuzi pia unapiga hatua kubwa.
  • Mageuzi ya shirika la IMF yatakiwa kuendelea kuinua kiwango cha sauti na uwakilishi wa makundi ya kiuchumi yanayojitokeza

  Kamati ya utendaji ya shirika la fedha la kimataifa IMF imetangaza kuwa imekubali ombi la kujiuzulu la mkurugenzi mkuu Bibi Christine Lagarde, na itaanzisha mara moja mchakato wa kumteua mkurugenzi mkuu mpya. Katika kipindi cha ukaguzi mkuu wa 15 wa mgao cha shirika hilo, mrithi wa Bibi Lagarde anatakiwa kufuata mwelekeo wa zama, kuhimiza mageuzi ya mgao na usimamizi ya shirika la IMF, kuendelea kuongeza sauti na uwakilishi wa makundi ya kiuchumi yanayojitokeza na nchi zinazoendelea, ili kulifanya shirika hilo kulinda uhalali na ufanisi wake.

  • Nchi za magharibi zatakiwa kujifunza uzoefu wa mapambano dhidi ya ugaidi wa Xinjiang

  Hivi karibuni mabalozi wa nchi 37 ikiwemo Russia, Saudi Arabia na Pakistan katika ofisi za umoja wa mataifa mjini Geneva, wametoa barua ya pamoja kwa mwenyekiti wa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa na mjumbe mwandamizi wa mambo ya haki za binadamu, ikipongeza maendeleo ya shughuli za haki za binadamu na mafanikio ya mapambano dhidi ya ugaidi na kazi za kuondoa msimamo mkali yaliyopatikana mkoani Xinjiang, China. Hii inamaanisha kuwa jumuiya ya kimataifa ina tathmini ya haki kwa maendeleo ya Xinjiang, na jaribio la baadhi ya nchi za magharibi kuilaumu Xinjiang na kuishinikiza China kwa kisingizio cha suala la "Haki za Binadamu" halitafanikiwa. Nchi hizo zinatakiwa kujifunza uzoefu wa Xinjiang katika mapambano dhidi ya ugaidi na kuutumia katika utatuzi wa masuala yao.

  • Uchumi wa China waendelea kwa utulivu

  Takwimu mpya zinazotolewa na idara ya takwimu ya taifa ya China zimeonesha kuwa, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu pato la taifa la China limezidi dola trilioni 6.5 za kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 6.3 ikilinganishwa na mwaka jana. Katika hali ambayo uchumi wa dunia unakabiliwa na hatua yz upande mmoja na kujilinda kibiashara, uchumi wa China umeendelea kwa utulivu na ukuaji wa uchumi huo una sifa ya juu zaidi.

  • China kuyawekea vikwazo makampuni ya Marekani yanayoiuzia silaha Taiwan ili kulinda kithabiti maslahi ya taifa
  • Uchambuzi: ongezeko la uwekezaji wa kigeni nchini China laonyesha kuwa kampuni za nje zina imani na uchumi wa China

  Takwimu zilizotolewa leo na Wizara ya Biashara ya China zinaonyesha kuwa katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, thamani ya mitaji ya kigeni iliyotumiwa nchini China ilifikia dola za kimarekani bilioni 70, kiasi ambacho kiliongezeka kwa asilimia 7.2 kuliko mwaka jana kipindi kama hicho. Wakati hatari ya uchumi wa dunia inaongezeka, na kasi ya ongezeko la uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni duniani inapungua, uwekezaji wa kigeni nchini China unaendelea kuongezeka, na hii imeonyesha kuwa kampuni za nje zina imani na uchumi wa China.

  • Viongozi wapya wa Umoja wa Ulaya watarajiwa kuhimiza uhusiano kati ya Umoja huo na China

  Rais Xi Jinping wa China leo amemtumia salama za pongezi waziri mkuu wa Ubelgiji Bw. Charles Michel kwa kuteuliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Baraza la Ulaya. Katika barua hiyo, rais xi amesema China inaunga mkono Ulaya kufanya kazi muhimu zaidi katika mambo ya kimataifa, na kupenda kuhimiza uhusiano wa kiwenzi kati ya pande hizo mbili katika masuala ya amani, maendeleo, mageuzi na ustaarabu.

  • Uchambuzi: Sababu tatu kuu zinaifanya dunia itegemee zaidi uchumi wa China

  Taasisi ya McKinsey Global imetoa ripoti ikisema kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2017, utegemezi wa dunia kwa uchumi wa China uliongezeka kutoka 0.4 hadi 1.2. Haya ni matokeo yanayotarajiwa ya maendeleo ya utandawazi duniani, na yameonyesha kuwa katika mchakato wa kujiunga na dunia, China imehimiza ukuaji wa uchumi wa dunia, na imani ya jumui ya kimataifa kwa uchumi wa China inaongezeka.

  • Uongo wa baadhi ya wanasiasa wa Uingereza kuhusu mambo ya Hong Kong
  Hivi karibuni tukio la kimabavu ambalo watu wenye msimamo mkali walivamia jengo la baraza la sheria lilitokea huko Hong Kong. Baadhi ya wanasiasa wa Uingereza wametumia taarifa ya pamoja ya China na Uingereza ambayo haifanyi kazi tena kama kisingizio, na kudai kuwa wanaunga mkono wakazi wa Hong Kong kulinda "uhuru" uliopiganiwa na Uingereza na kuitaka serikali ya mkoa wa utawala maalumu la Hong Kong kutotumia tukio hilo la kimabavu kama sababu ya kutuliza hali. Madai hayo yasiyo na msingi wowote yanaunga mkono kidhahiri uhalifu na vitendo vya kimabavu na kuingilia kati mambo ya Hong Kong na siasa ya ndani ya China, ambayo yanaweza kuharibu uhusiano kati ya China na Uingereza.
  • Ushirikiano kati ya China na Marekani ni matarajio ya wananchi wa nchi hizo mbili

  Gazeti la Marekani Washington Post limetoa barua wazi kwa rais Donald Trump wa Marekani na bunge la Marekani. Barua hiyo iliyosainiwa na watu mia moja kutoka sekta ya taaluma, diplomasia, jeshi na biashara nchini Marekani, imeeleza ufuatiliaji kwa kupungua kwa uhusiano kati ya Marekani na China, huku ikiona hali hiyo hailingani na maslahi ya Marekani na Ulimwengu. Barua hiyo pia imesema, hakuna makubaliano ya pamoja ya kupambana kwa pande zote na China kwenye serikali ya Marekani, na kubainisha matarajio ya kuendeleza uhusiano huo kati ya nchi hizo mbili nchini Marekani.

  • China kutekeleza kwa hatua madhubuti ahadi kuhusu kupanua ufunguaji mlango

  Baada ya rais Xi Jinping wa China kutangaza hatua tano muhimu za kuharakisha hatua ya kupanua ufunguaji mlango kwenye Mkutano wa kilele wa kundi la G20, serikali ya China imeonesha nia thabiti ya kupanua ufunguaji mlango katika mkutano wa 13 wa Baraza la Davos la majira ya joto, na itakuza hatua ya ufunguaji mlango katika viwanda vya utengenezaji na utoaji wa huduma, kupunguza zaidi kiwango cha ushuru, kulinda kwa nguvu zaidi hakimiliki ya ubunifu, na kiwango cha ufunguaji mlango na uwazi kwa uwekezaji kutoka nje pia kitakuwa juu zaidi.

  • Jaribio lolote la kuingilia mambo ya Hong Kong na siasa za ndani za China halitafanikiwa

  Julai 1 ambayo ni maadhimisho ya miaka 22 tangu Hong Kong irudi China, baadhi ya watu wenye msimamo mkali walishambulia jengo la Bunge la Hong Kong, na kufanya uharibifu mbaya ndani ya jengo hilo. Tukio hilo la kimabavu limeathiri vibaya utawala wa sheria na kuharibu vibaya utulivu wa jamii ya Hong Kong, ambalo linalaaniwa na jumuiya ya kimataifa. Lakini Marekani, Uingereza na Umoja wa Ulaya zimetumia kisingizio cha uhuru na haki za binadamu kudai kuhakikisha haki za kupinga kwa njia ya amani. Kigezo tofauti cha kushughulikia uhalifu wa kimabavu ni kitendo kibaya cha kuingilia kati mambo ya Hong Kong na siasa za ndani ya China, ambacho kinalaaniwa na kupingwa kithabiti na serikali ya China.

  • China yatangaza Hatua mpya za usimamizi kuhusu masharti ya uwekezaji kwa kampuni kutoka nje
  Serikali ya China jana ilitangaza rasmi Hatua maalumu za usimamizi kuhusu masharti ya uwekezaji kwa kampuni za kigeni, pamoja na Hatua maalumu za usimamizi kuhusu masharti ya uwekezaji wa kampuni hizo kwenye Eneo la Biashara Huria, ikiwaruhusu wafanyabiashara kutoka nje kuwekeza kwa upande wake pekee katika sekta nyingi zaidi nchini China.
  • Mali za China zimekuwa sehemu muhimu za mitaji ya kimataifa

  Baada ya soko la hisa la China kufungwa leo, kampuni ya kutunga vigezo ya pili kwa ukubwa duniani FTSE Russell imeweka Hisa A ambayo ni hisa ya RMB katika mfululizo wa vigezo vya hisa kote duniani. Hii ni habari nyingine njema kwa soko la mitaji la China baada ya kampuni kubwa zaidi ya kutunga vigezo duniani MSCI kuinua kiwango cha Hisa A. Hii inamaanisha kuwa wawekezaji wa kimataifa sio tu wanaendelea kudumisha mahitaji ya uwekezaji kwa soko la mitaji la China, bali pia wana imani na mustakabali wa uchumi wa China.

  • China na Marekani zinaweza kutatua mgogoro wao wa kibiashara kama zikifanya mazungumzo kwa usawa

  Marais wa China na Marekani Jumanne walizungumza kwa njia ya simu, wakisema watakutana tena kwenye mkutano wa wakuu wa kundi la G20 mjini Osaka, Japan. Pia wamekubaliana kudumisha mawasiliano kati ya timu za biashara za pande hizo mbili. Habari hii ilituliza kwa kiasi wasiwasi wa watu na kulipa nguvu soko la hisa duniani.

  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako