• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Jumuiya ya nchi za kiarabu na Umoja wa Ulaya zaimarisha ushirikiano ili kukabiliana na changamoto

  Mkutano wa kwanza wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu na Umoja wa Ualya umefungwa huko Sharm el Sheikh, nchini Misri, na kuhudhuriwa na viongozi zaidi ya 50 kutoka nchi za kiarabu na za Ulaya. Mafanikio yaliyopatikana kwenye mkutano huo yameonesha kuwa taasisi hizo mbili kubwa za kikanda zina makubaliano mengi zaidi ya pamoja kuliko tofauti.

  • China na Marekani zinatakiwa kuendelea kufanya juhudi ili kupanua maslahi yao zaidi

  Duru ya saba ya mazungumzo ya ngazi ya juu ya kibiashara kati ya China na Marekani yalimalizika tarehe 24 Jumapili mjini Washington. Kwenye mazungumzo hayo ya siku nne, pande mbili zimekubaliana kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa nchi mbili walipokutana nchini Argentina, na kupata maendeleo halisi juu ya masuala ya uhamisho wa teknolojia, ulinzi wa haki miliki ya ubunifu, vizuizi visivyo ushuru, sekta za huduma na kilimo, kiwango cha ubadilishanaji wa fedha na mengineyo. Wakati huohuo, rais Donald Trump wa Marekani amesema kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa ataahirisha mpango wa kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China zitakazoingizwa Marekani uliopangwa kuanza tarehe mosi mwezi Machi.

  • China na Marekani zina maslahi ya pamoja katika ulinzi wa hakimiliki za ubunifu

  Mazungumzo ya ngazi ya juu ya kibiashara kati ya China na Marekani yanayoendelea mjini Washington, Marekani yamepiga hatua chanya katika masuala ya uwiano wa biashara, kilimo, utoaji wa teknolojia, ulinzi wa hakimiliki za ubunifu, huduma za kifedha na mengineyo. Kati ya masuala hayo, nchi hizo mbili zimeafikiana zaidi katika ulinzi wa hakimiliki za ubunifu, kwani zina maslahi mengi ya pamoja katika suala hilo.

  • Hatua kubwa yapigwa mbele katika mjadala wa China na Marekani
  Mjadala wa 6 wa ngazi ya juu kuhusu mambo ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani ulimalizika jana hapa Beijing. Kwa mara ya kwanza rais Xi Jinping wa China alikutana na ujumbe wa Marekani tangu hali ya mvutano ianze kupanda ngazi mwezi Februari mwaka jana.
  • Rais wa China akutana na mjumbe wa biashara wa Marekani
  • Mustakabali mzuri wa soko la China wavutia uwekezaji kutoka nchi za nje
  Wizara ya Biashara ya China imetangaza kuwa, mwaka 2018 China imejenga kampuni 60,533 zinazowekezwa na wafanyabiashara nchini China, likiwa ni ongezeko la asilimia 69.8; matumizi ya fedha yamefikia dola za kimarekani bilioni 130.2, likiwa ni ongezeko la asilimia 0.9. Mwaka jana wakati dunia nzima ilipokabiliwa na changamoto za kuvutia fedha za kigeni, China ilipata ongezeko kubwa katika sekta hiyo, hali ambayo imeonesha mustakabali mzuri wa soko la China.
  • Matumizi ya fedha ya wananchi wa China yapata maendeleo makubwa wakati wa Sikukuu ya Spring
  Takwimu mbalimbali kuhusu mapumziko ya sikukuu ya Spring zimetolewa leo.
  • Watalii kutoka China watilia nguvu ya uhai duniani

  Mashirika husika ya utalii nchini China hivi karibuni yalikadiria kuwa, kwenye kipindi cha sikukuu ya Spring ya mwaka 2019 nchini China, idadi ya wachina watakaotalii nchi nyingine itafikia milioni 7, na kuongezeka kwa asilimia 15 kuliko mwaka 2018. Thailand, Japan na Indonesia na nchi jirani zimekaribishwa zaidi na wachina. Mkurugenzi wa Baraza la utalii duniani (WTTC) anayeshughulikia sera na matangazo Bw. Olivia Ruggles Brise alisema, kuongezeka kwa wachina wanaoweza kubeba gharama za utalii kumehimiza masoko ya nchi jirani ya utalii ya China zikiwemo Bangkok na Jakarta. Ofisa mtendaji wa kampuni moja ya kimataifa ya hoteli Bw. James Riley alisema, amezingatia mabadiliko ya tabia za utalii wa wachina, zamani watalii wa China walikuwa wananunua bidhaa tu, lakini hivi sasa wanapenda kuona utamaduni zaidi.

  • China na Marekani yazindua njia mpya ya kutatua suala katika mazungumzo yao ya biashara

  Mazungumzo ya ngazi ya juu ya biashara kati ya China na Marekani yalimalizika Alhamisi mjini Washington. Kwa siku mbili, chini ya maelekezo ya makubaliano muhimu yaliyofikiwa na marais wa nchi hizo mbili, pande hizo zimefanya majadiliano mahususi, ya dhati, na ya kiujenzi kuhusu mada zinazofuatilia kwa pamoja, ikiwemo uwiano wa biashara, usafirishaji wa teknolojia, ulinzi wa haki miliki za ubunifu, vizuizi visivyo vya ushuru, huduma, kilimo na mfumo wa utekelezaji. Pia pande hizo mbili zimepanga utaratibu wa majadiliano yajayo na ratiba.

  • China yapiga hatua muhimu katika kuhimiza ufunguaji mlango wa kimfumo

  Bunge la umma la China ambalo ni shirika la utungaji wa sheria la China limeanza kufanya ukaguzi wa mara ya pili kwa Sheria ya uwekezaji wa wafanyabiashara wa kigeni kuanzia leo, hatua ambayo imeonesha China inadhamiria kukamilisha na kutangaza mapema sheria hiyo, ambayo pia ni hatua muhimu kwa China kufanya ufunguaji mlango wa kimfumo.

  • China yahimiza ufunguaji mlango kwenye kiwango cha juu zaidi kwa njia ya uoanishaji wa mifumo

  Katika Mkutano wa mwaka 2019 wa Baraza la Uchumi Duniani WEF uliofanyika wiki iliyopita, China imeonesha kwa mara nyingine tena nia na imani ya kusukuma mbele kwa pande zote ufunguaji mlango kwa nje. Katika mwezi mmoja uliopita, mkutano wa kazi ya uchumi wa Kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China umetangaza kwa mara ya kwanza kuwa, itahimiza ufunguaji mlango wa kimfumo kutoka kwenye sekta za bidhaa. Hayo yote yanamaanisha kuwa ufunguaji mlango wa China kwa nje utaingia kwenye kipindi kipya.

  • Kampuni ndogondogo nchini China zina fursa ya kupunguza kodi zao

  Mwanzoni mwa mwaka huu, serikali ya China ilitangaza sera mpya mfululizo ili kutia nguvu ya uhai sokoni, na kukabiliana na shinikizo la kupungua kwa ongezeko la uchumi. Sera iliyotangazwa kwanza ni kupunguza kodi za kampuni ndogondogo ili kuzinufaisha, ambayo itatekelezwa kwa miaka mitatu. Sera hiyo imechukuliwa kuwa mwanzo wa sera mfululizo zitakazotekelezwa na serikali ya China mwaka huu katika kupunguza kodi, na itahimiza maendeleo ya uchumi wa China.

  • Matokeo mazuri ya mwisho kupatikana kutokana na juhudi za pamoja za China na Marekani

  Mazungumzo ya ngazi ya naibu mawaziri kati ya China na Marekani kuhusu suala la uchumi na biashara yalifungwa jana mjini Beijing. Haya ni mazungumzo ya kwanza ya ana kwa ana kati ya pande hizo mbili kwa ajili ya kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili nchini Argentina.

  • Hotuba ya rais Xi kuhusu suala la Taiwan ni mwongozo mpya kwa amani, muungano na maendeleo ya China
  Hivi karibuni rais Xi Jinping wa China alitoa hotuba muhimu kuhusu uhusiano kati ya China bara na kisiwa cha Taiwan, akisema kutimiza muungano kamili wa China ni jukumu muhimu la kihistoria kwa Chama cha kikomunisti cha China, serikali ya China na wananchi wake, na kusisitiza kuwa kwenye mchakato wa kustawisha upya taifa la China, ni lazima na pia ni hakika muungano wa nchi utimizwe.
  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako