• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Hali ya haki za binadamu nchini Marekani yawekwa wazi katika ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini humo

  Leo ni Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu. Hali ya haki za binadamu nchini Marekani imewekwa wazi katika ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini humo.

  • Kwa nini vyombo vya habari vya magharibi vinakaa kimya kuhusu filamu za kumbukumbu kuhusu Xinjiang

  Shirika kuu la Utangazaji la China CMG hivi karibuni limetoa filamu mbili za kumbukumbu kuhusu mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea mkoani Xinjiang, China, mashambulizi ambayo yamedhuru vibaya haki za binadamu za watu wa makabila mbalimbali mkoani humo. Filamu hizo zimefuatiliwa sana na watu, ila zimepuuzwa na vyombo vya habari vya nchi za magharibi. CMG imetoa tahariri yenye kichwa cha "Kwa nini vyombo vya habari vya magharibi vinakaa kimya kuhusu filamu za kumbukumbu kuhusu Xinjiang".

  • Xinjiang yaondoa ugaidi kwa kuimarisha utulivu na ustawi

  Baraza la wawakilishi la bunge la Marekani limetoa Mswada wa mwaka 2019 wa Sera ya Haki za Binadamu za Wauyghur, na kupaka matope sera ya serikali ya China katika mkoa wa Xinjiang. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri yenye kichwa cha "Xinjiang yaondoa ugaidi kwa kuimarisha utulivu na ustawi."

  • China yapiga hatua thabiti katika kuelekea kuwa nchi yenye nguvu kubwa kibiashara
  Hivi karibuni China ilitangaza Mwongozo kuhusu kuhimiza maendeleo yenye sifa bora ya biashara, ikiweka mipango kuhusu kuzidi kuboresha muundo na kuongeza ufanisi na uwezo wa biashara, ili kutimiza maendeleo yenye sifa bora ya biashara na kuielekeza China kuwa nchi yenye nguvu kubwa ya biashara…
  • China haitashindwa na tishio lolote la nje

  Serikali ya Marekani hivi karibuni imesaini "Mswada wa Haki za Binadamu na Demokrasia ya Hong Kong" na kuuidhinisha kuwa sheria, ili kuunga mkono watu wenye msimamo mkali wanaovuruga utulivu mkoani Hong Kong. Kitendo hicho kimeingilia kati mambo ya Hong Kong, ambayo ni mambo ya ndani ya China, na kukiuka sheria ya kimataifa na kanuni ya kimsingi ya uhusiano wa kimataifa. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri inayosema China haitashindwa na tishio lolote la nje.

  • Mswada wa Marekani kuhusu suala la Hong Kong ni mchezo wa kisiasa

  Utawala wa Marekani jana ulisaini "Mswada wa Haki za Binadamu na Demokrasia ya Hong Kong" na kuuidhinisha kuwa sheria. Kitendo hiki cha kuingilia kati mambo ya Hong Kong ambayo ni mambo ya ndani ya China kimepingwa vikali na China na jumuiya ya kimataifa. Shirika kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri yenye kichwa cha "Mswada wa Marekani kuhusu Suala la Hong Kong ni Mchezo wa Kisiasa"

  • Ziara ya rais wa China nchini Ugiriki yasaidia kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo

  Rais Xi Jinping wa China amefanya ziara nchini Ugiriki kuanzia tarehe 10 hadi 12. Katika ziara yake hiyo, viongozi wa nchi hizo mbili wamejadiliana kuhusu jinsi ya kuongeza kuaminiana kisiasa, kuimarisha ushirikiano wa kivitendo, kuhimiza mazungumzo kuhusu ustaarabu, na kufikia maoni muhimu ya pamoja na matunda mengi. Hii imeonesha kuwa majadiliano ya kiustaarabu na ushirikiano wa kunufaishana vinainua ngazi ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Ugiriki, jambo litakalowaletea watu wa nchi hizo fursa za maendeleo na kukuza uhusiano kati ya China na Ulaya.

  • "Siku ya Manunuzi ya Novemba 11" yathibitisha uhai mkubwa wa uchumi wa China

  Tarehe 11 Novemba ni "Siku ya Manunuzi" ambayo iliwadia siku moja baada ya Maonesho ya Pili ya Kimataifa ya Uingizaji wa Bidhaa za Nje ya China. Katika siku hiyo, thamani ya mauzo ya bidhaa kupitia Taobao na Jingdong ambayo ni makampuni makubwa ya mauzo kupitia mtandao wa Internet nchini China ilizidi dola bilioni 38.3 na 29.2 za kimarekani. Shirika kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri yenye kichwa cha habari "Mauzo mazuri ya Siku ya Manunuzi ya Novemba 11 yathibitisha uhai mkubwa wa uchumi wa China.

  • CIIE yahimiza kufungua mlango na maendeleo kwa pamoja

  Maonesho ya pili ya Kimataifa ya Uingizaji wa Bidhaa kutoka Nje ya China CIIE yamefungwa mjini Shanghai, China, baada ya kufikiwa kwa makubaliano ya biashara yenye thamani ya dola bilioni 71.13 za kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 23 ikilinganishwa na mwaka jana. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri ya "CIIE yahimiza kufungua mlango na maendeleo ya pamoja".

  • Maonesho ya kimataifa ya bidhaa zinazoagizwa na China yaonesha mivuto minne ya soko la China

  Maonesho ya pili ya kimataifa ya bidhaa zinazoagizwa na China yanafanyika mjini Shanghai, China. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri ya "maonesho ya kimataifa ya bidhaa zinazoagizwa na China yaonesha mivuto minne ya soko la China".

  • China na Marekani zahimiza utatuzi wa mvutano wa kibiashara

  • Pendekezo la China lachangia ujenzi wa mustakabali wa pamoja katika mtandao wa Internet
  Mkutano wa sita wa Mtandao wa Internet duniani umefunguliwa leo mjini Wuzhen, mkoani Zhejiang, China.
  Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi ambayo ilichambua kwa kina mustakabali wa maendeleo ya mtandao wa Internet, na kudhihirisha kuwa ni jukumu la pamoja kwa jumuiya ya kimataifa kuendeleza, kutumia na kusimamia vizuri mtandao wa Internet ili kuufanya uhudumie vizuri binadamu.
  • Uchumi wa China waendelea kwa utulivu ingawa unakabiliwa na changamoto

  Takwimu zilizotolewa leo na Idara Kuu ya Takwimu ya China zinaonesha kuwa, katika robo tatu za mwanzo mwaka huu, pato la taifa la China GDP limezidi dola za kimarekani trilioni 9.87, na kuongezeka kwa asilimia 6.2 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hiki.

  • China yaonesha imani ya kiuchumi kwa kufungua zaidi sekta ya fedha

  Serikali ya China imeamua kurekebisha sheria kuhusu usimamizi wake kwa makampuni ya nje ya bima na benki, ili kufungua mlango zaidi kwa sekta ya fedha, hatua inayoonesha imani ya China kuhusu uchumi wake, na pia italeta injini mpya kwa ukuaji wa uchumi wa dunia.

  • Marekani kujidhuru kimaslahi kwa kuingilia mambo ya Hong Kong

  Baraza la chini la bunge la Marekani jana lilipitisha "Mswada wa sheria wa mwaka 2019 kuhusu haki za binadamu na demokrasia ya Hong Kong", likiunga mkono watu wenye msimamo mkali na wanaofanya vurugu mkoani Hong Kong, China. Kitendo hicho si kama tu kimekiuka sheria za kimataifa na kuingilia mambo ya ndani ya China, bali pia kitadhuru maslahi ya Marekani.

  • China na Marekani zasuluhisha mvutano wa kibiashara kwa njia mwafaka

  Duru mpya ya mazungumzo ya ngazi ya juu kati ya China na Marekani kuhusu suala la kibiashara imefanyika hivi karibuni mjini Washington, na kupiga hatua halisi katika sekta mbalimbali zikiwemo kilimo, ulinzi wa hakimiliki za kiubunifu, kiwango cha ubadilishaji wa fedha, huduma za kifedha, kupanua ushirikiano wa kibiashara, utoaji wa teknolojia, na utatuzi wa migongano. Pande hizo mbili zitaendelea na mazungumzo hayo ili kufikia makubaliano ya mwisho.

  • China siku zote inalinda usalama wa chakula duniani
  • Kuendeleza biashara za huduma kunahitaji kuimarisha ushirikiano wa kimataifa
  • Ongezeko la hatari ya uchumi wa dunia lahitaji kuimarisha utaratibu wa dunia yenye ncha nyingi
  • China yadumisha uwezo mkubwa wa ushindani duniani
  Ripoti kuhusu uwezo wa ushindani duniani ya mwaka 2019 iliyotolewa leo kwenye Baraza la Uchumi Duniani huko Geneva, Uswis, imeonesha kuwa, China inashika nafasi 28 kutokana na uwezo wa ushindani.
  prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 next
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako