• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • • Valentine day 2012-02-14
    Siku ya wapendano inayojulikana kwa kimombo Valentine's day huwa ni February 14 ya kila mwaka, na mwaka huu kama kawaida inasubiriwa kwa hamu na wale walio kwenye mahusiano ya kimapenzi, kuliko yale ya kifamilia.
    • Mwaka mpya wa jadi wa China 2012-01-26
    Waswahili wanasema mambo mengi yana fanana hapa Duniani, kama halipo hapa basi lipo huko au kule, na hilo ndilo linalosemwa kwenye baadhi ya mambo ya jamii tofauti hapa duniani toka tabia moja hadi nyingine.
    • Elimu ya China 2011-11-23
    Waswahili wanasema, usicheze na elimu maana ndio mkombozi wako siku za baadae. Ni kweli, elimu imewakomboa wengi hapa duniani. Kwa kuzingatia hilo, CHINA imeamua kulisaidia bara la AFRICA katika suala la elimu.
    • Mapenzi 2011-11-22
    Kuna msemo katika vitabu vya dini usemao binadamu tumeletwa ilituijaze duniani, kuifanya ipendeze na yenye mvuto kila wakati, na pia kuna msemo wa wahenga usemao duniani wawili wawili ukiwa na maana kuwa mwanaume anpofikia umri Fulani anahitajika kuoa na mwanamke kadhalika aolewe.
    • Majina 2011-11-22
    Moja ya kitu ambacho kimenivutia sana hapa nchini China ni kwa kila kitu kutamkwa kwa lugha yao hakuna jina au sehemu inayotamkwa kwa lugha ya kigeni wao wanatamka kwa lugha yao ya Kichina tu tena kwa rafuzi zao na inaleta mvuto. Na sio hivyo tu kutamka hata wageni wanaokuja kufanya kazi hapa au kusoma basi majina yao yanatafsiliwa kwa lugha ya Kichina ili kuleta urahisi kwa wazawa kumjua rahisi muhusika hilo nimelipenda.
    • Urafiki kati ya China na Afrika 2011-11-22
    Urafiki kati ya China na nchi za Kiafrica unazidi kukua kila mwaka, na umekuwa wa mafanikio makubwa kuliko kitu kingine chochote hasa kwa nchi hizo za barani Africa. Kwa wanaotoka Tanzania na Zambia wanajua sana umuhimu wa urafiki baina ya China na Africa hasa kutokana na Reli ya Tazara ambayo hadi leo inatumiwa na nchi mbili hizo na imekuwa ni kichocheo kikubwa cha maendelea kwa wananchi wa nchi hizo.
    • Kazi 2011-06-08
    Kule nchini Tanzania hasa ukanda wa pwani mara nyingi wanasema kazi ni kazi tu ili mradi mkono uende kinywani, lakini pia nchini humo kuna mgao wa kazi utasikia hii kazi ya kiume au hii kazi ya kike.
    • Lugha ya Kichina 2011-05-06
    Lugha ya kichina kwa sasa ni moja ya lugha inayokuwa kwa kasi hapa duniani hasa kutokana na Taifa lake kuzidi kukuwa kiuchumi na kuwa kivutio kwa wengi duniani. Kuna watu wengi hivi sasa wanaojifunza lugha hii wakiwa ndani ya China na wengine nje ya China na wengi wao wanaojifunza lugha hii ni kutoka kwenye mataifa ya nchi zinazoendelea hasa barani Afrika. Hii ni kutokana na nchi hiyo kujikita sana kwenye bara hilo kwenye mambo ya uwekezaji na kuongeza ajira.
    • Makala ya nne 2011-04-20
    Kuaizi au kwa Kiswahili unaweza kutamka kwaizi ni chombo maarufu sana hapa nchini China hasa unapokuja kwenye swala la kula, kuaizi zimekuwa ni kivutio kikubwa mno kwa wageni wengi wanaoingia katika nchi hii ya Mashariki ya mbali.
    • Makala ya tatu 2010-12-24
    Sikukuu ya Christmas au Noel kwa lugha yangu ya Kiswahili ni maarufu kila kona hapa na duniani. Hapa nchini China sikukuu hii inaitwa Shengdanjie. Wenyeji wangu wamenifahamisha kuwa Wachina wengi hawasherehekei sikukuu hii, kwa wana sherehe yao inayokuja mwezi Januari 2011 ambayo ni kubwa zaidi, lakini vijana wa China hivi leo wanafurahia sana sikukuu hiyo...
    • Makala ya pili 2010-12-04
    Ni men hao?.. Kwanza leo napenda nianze kwa kuwasalimia kwa kichina kuonesha kwamba hata sisi waafrika tunaweza kujifunza na kuongea kichina, lugha ambayo waafrika tunaiona kuwa ni miongoni mwa lugha ngumu hapa duniani. Ninakumbuka nyumbani Tanzania kuna msemo unaosema "lugha ya mtu ni lugha ya mtu tu" au "lugha ya wenyewe ni ya wenyewe tu".
    • Makala ya kwanza 2010-11-20
    Ama kweli ughaibuni kuna mambo na nyumbani ni nyumbani tu. Wahenga walisema hivyo, lakini huwezi kuamini hadi uende mbali na nyumbani, ndio utakumbuka kuwa nyumbani ni nyumbani tu. Nakumbuka nilipoondoka Dar es salaam kuja Wuhan, China nilikuwa mwenye furaha sana...
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako