Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
Mandhari nzuri kwenye msitu wa mawe ulioko mkoani Yunnan nchini China 2007/07/16
Kwenye mkutano wa 31 wa kimataifa kuhusu urithi wa dunia uliofanyika huko Christchurch, New Zealand, ombi kuhusu "ardhi ya chokaa ya sehemu ya kusini mwa China" ikiwa ni pamoja na msitu wa mawe wa mkoani Yunnan, tunda la Litch pamoja na Wulong ya mji wa Chongqing, zilipita kwenye ukaguzi na upigaji kura, na zimeorodheshwa kuwa urithi wa dunia, na kuwa sehemu ya 34 ya urithi wa duni? wa nchini China
Mji wa Chongqing wenye milima na mito ya kupendeza 2007/07/02
Kati ya sehemu maarufu za utalii za nchini China, pengine umewahi kusikia "Magenge Matatu" ya mto Changjiang na "Sanamu yenye Miguu Mikubwa", ambazo ziko katika mji wa Chongqing. Mji wa Chongqing, ambao ulifanywa kuwa mji unaosimamiwa moja kwa moja na serikali kuu miaka michache iliyopita, unavutia idadi kubwa ya watalii kutokana na sehemu zake nyingi zenye mandhari nzuri ya kimaumbile pamoja na utamaduni wa jadi.
Kutembelea "Jumba la makumbusho la ikolojia ya makabila" mkoani Guizhou 2007/06/18
 Kwenye mkoa wa Guizhou ulioko sehemu ya kusini magharibi mwa China, wanaishi watu wa makabila madogo 48. Serikali ya mkoa wa Guizhou ikizingatia umaalumu wa kuweko kwa makabila mengi madogo, ilijenga majumba manne ya makumbusho yasiyo na uzio, ambayo yanawafahamisha watalii wa nchini na wa nchi za nje kuhusu utamaduni maalumu na desturi na mila za wakazi wa makabila madogo.
Bustani ya jiolojia ya dunia iliyoko mkoani Helongjiang  2007/06/04
Katika kipindi hiki cha leo tunawaletea maelezo kuhusu bustani ya jiolojia yenye maziwa matano yanayopakana mkoani Helongjing, sehemu ya kaskazini mashariki mwa China. Sehemu hiyo inaitwa na wanasayansi kuwa ni "jumba la makumbusho ya volkano" ya dunia kutokana na sehemu hiyo kuwa na volkano nyingi zilizo hai
Kutembelea vijiji vya mji wa Jian, mkoani Jiangxi 2007/05/21
Hivi sasa ni majira ya Spring nchini China, ambapo hali ya hewa inaanza kubadilika kuwa joto, na maua yanachanua, ikiwa unataka kuitembelea China hivi sasa, basi ni vizuri utembelee kwenye sehemu ya vijiji ya mji wa Jian, mkoani Jiangxi. Kwenye sehemu ya vijiji ya mji wa Jian, si kama tu utaweza kushiriki kwenye shughuli za kilimo shambani na kushiriki kwenye mashindano ya mbio ya mashua, bali pia unaweza kuonja vitoweo vyenye umaalumu wa sehemu ya vijiji.
Mji wa Hangzhou  2007/05/07
Mji wa Hangzhou uliopo mashariki mwa China unasifiwa kuwa ni mji ulio kama peponi. Mji huo ni mji wa kale, ambapo Ziwa Xihu lililoko katikati ya mji huo linaufanya mji huo uonekane kuwa na utulivu zaidi.
Kujiburudisha kwa vitoweo vya mboga mjini Beijing 2007/04/23
Chakula cha mboga kikiwa ni moja ya mitindo ya maisha ya afya, kinazidi kupendwa na watu wengi. Katika kipindi hiki cha leo tutawafahamisha kuhusu migahawa miwili maalumu ya chakula cha mboga iliyopo hapa Beijing. Mgahawa unaoitwa "Putiyuan" ni mgahawa maarufu na wenye umaalumu wa kipekee kati ya migahawa ya vyakula vya mboga mjini Beijing.
Hakelu lililojengwa likining'inia 2007/04/09
Katika kipindi hiki kwa leo, nitawafahamisha hekalu lililojengwa kwenye genge la mlima, hekalu hilo linajulikana kwa Xuankongsi, maana yake katika Kichina ni hekalu lilikotundikwa angani, na liko kwenye bonde moja wilayani Hunyuan.
Kutalii kwenye bonde la Zhangbu mkoani Guizhou 2007/03/26
Mandhari nzuri ya mawe yenye maumbo ya ajabu, mashimo yenye maji ya kina kirefu pamoja na miti mbalimbali ya kupendeza kwenye bonde la Zhangbu lililoko katika wilaya ya Pingtang mkoani Guizhoi, sehemu ya kusini magharibi mwa China inawavutia watalii wengi.
Matembezi ya kuangalia vyungu katika mji wa Jieshou, mkoani Anhui 2007/03/12
Ufundi wa jadi wa utengenezaji wa vyungu wa mji wa Jieshou, mkoa wa Anhui ulioko sehemu ya kati mwa China ulianza zaidi ya miaka elfu moja iliyopita. Vyungu hivyo vinafinyangwa kwa udongo wa mfinyanzi, kupakwa rangi na kuchomwa moto katika tanuri.
1 2 3 4 5 6 7 8 9 10