Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
 
  • Makampuni binafsi nchini China yawapatia Wachina nafasi nyingi za ajira
  •  2007/07/10
    Kutokana na maendeleo ya kasi ya makampuni binafsi nchini China, hivi sasa makampuni binafsi yamekuwa nguvu muhimu ya kutoa nafasi za ajira. Kuanzia mwaka 2001 hadi mwaka 2006, makampuni binafsi yamekuwa yanatoa nafasi mpya za ajira milioni 5 hadi milioni 6 kwa mwaka, ambazo zinachukua robo tatu ya nafasi mpya za ajira mijini, hivyo makampuni binafsi yanafuatiliwa na watu wengi zaidi.
  • Viwanda vya magari vyenye hakimiliki ya ubunifu vya mkoa wa Anhui vyaendelea kwa kasi
  •  2007/06/26
    Walikuwepo wataalam wa kiuchumi waliosema kuwa viwanda vya magari ni "uti wa mgongo wa viwanda", kwa maana fulani viwanda vya magari vinaonesha kiwango cha viwanda vya nchi. Katika miaka ya hivi karibuni, China pia inafanya juhudi kuendeleza viwanda vya magari, hasa kutilia maanani kuendeleza viwanda vya utengenezaji magari yenye hakimiliki ya ubunifu, na mkoa wa Anhui ulioko katikati ya China unaongoza katika sekta hiyo
  • Ujenzi wa miji yenye eneo kubwa misitu wapata maendeleo
  •  2007/06/05
    Katika hali ya kawaida, misitu iko kwenye sehemu za milimani ambazo ziko mbali na miji, ambayo ni nadra inaonekana mijini. Lakini katika miaka ya hivi karibuni, upandaji wa miti mijini unavuma sana katika miji mingi nchini China ili kuboresha mazingira ya kuishi.
  • Supamaketi zaanzisha katika vijiji vingi nchini China
  •  2007/05/22
    Zamani nchini China kulikuwa na usemi mmoja unaohusu njia ya kununua bidhaa kwa wakulima, yaani "kununua viungo kwenye vijiji vyao, kununua vitu kwa matumizi ya kila siku kwenye magulio, na kununua bidhaa kubwa katika miji ya wilaya".
  • Mabadiliko mapya yaliyotokea kwenye maonesho ya 101 ya kimataifa ya bidhaa zinazosafirishwa nje na zinazoagizwa kutoka nje ya China
  •  2007/05/08
    Maonesho ya kimataifa ya bidhaa zinazosafirishwa nje ya China ni maonesho maarufu ya kimataifa ya bidhaa. Maonesho hayo yanafanyika katika majira ya mchipuko na majira ya mpukutiko kila mwaka mjini Guangzhou. Mpaka sasa yamefanyika kwa miaka 50.
  • Majaribio mapya ya mageuzi ya mambo ya fedha vijijini nchini China
  •  2007/04/24
    Mageuzi ya mambo ya fedha vijijini ni sehemu muhimu ya mageuzi ya mambo ya fedha nchini China. Katika miaka ya hivi karibuni, idara ya usimamizi wa fedha ya China imekuwa inarekebisha sera ya kuingia kwa idara za fedha za benki vijijini, na kuhimiza mitaji mbalimbali kuingia katika idara za fedha vijijini, ili kuwasaidia wakulima milioni 800 kuongeza mapato yao haraka. Wakati huohuo idara za aina mpya za fedha zinazofaa vijiji pia zinatokea vijijini.
  • Mji wa Wuxi waendeleza chapa zenye historia ndefu
  •  2007/04/10
    Mji wa Wuxi ulioko kusini mashariki mwa China ni chimbuko la shughuli za viwanda na biashara ya kitaifa ya zama za karibuni nchini China. Bidhaa za chapa nyingi maarufu zenye historia ndefu zinatengenezwa mjini humo. Chapa hizo ambazo zilianzishwa kwa juhudi na busara za watu wa vizazi kadhaa, ni mali zisizopatikana kwa urahisi.
  • China yafanya juhudi ili kukamilisha mfumo wa mambo ya fedha vijijini
  •  2007/03/27
    Kikilinganishwa na miji na sehemu zinazoendelea kwa kasi kiuchumi, kiwango cha utoaji huduma za fedha katika vijiji vya China ni cha chini, hali ambayo inasababisha ukosefu wa fedha kwa ajili ya maendeleo ya sehemu za vijiji.
  • Mkoa wa Qinghai wajaribu kuwa na mtizamo mpya wa kuwasaidia watu maskini kuanzisha shughuli iil kuondokana na umaskini
  •  2007/03/13
    Mkoa wa Qinghai uko kwenye uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet, kaskazini magharibi mwa China. Ingawa mkoani humo kuna maliasili nyingi, lakini kutokana na kuwa na idadi ndogo ya watu, na kutokuwa na hali nzuri ya mawasiliano, ukilinganishwa na sehemu zilizoendelea za mashariki mwa China, mkoa huo ni sehemu ambayo bado haijaendelea kiuchumi, na idadi ya watu maskini mkoani humo bado ni kubwa
  • Waziri mkuu wa China atoa ripoti ya kazi za serikali
  •  2007/03/07
    Mkutano wa mwaka wa Bunge la umma la China umefunguliwa tarehe 5 Machi asubuhi hapa Beijing, ambapo waziri mkuu wa China Bwana Wen Jiabao ametoa ripoti ya kazi za serikali.
  • China itaharakisha utafiti wa miradi muhimu ya sayansi na teknolojia
  •  2007/02/20
    Mkutano wa taifa kuhusu teknolojia na sayansi uliofanyika kwa siku mbili, ulifungwa tarehe 30 mwezi Januari hapa Beijing. Habari kutoka kwenye mkutano zimesema, serikali ya China imeweka kipaumbele katika miradi 16 muhimu ya teknolojia na sayansi ukiwemo utafiti wa ndege kubwa, utafiti na matumizi ya raslimali za baharini na teknolojia ya nishati endelevu
  • Athari ya kampuni za China yaanza kuonekana katika biashara ya mali-ghafi duniani
  •  2007/02/13
    Siku chache zilizopita kampuni ya chuma na chuma cha pua ya Baoshan, ambayo inachukua nafasi ya kwanza kwa ukubwa miongoni mwa kampuni za chuma na chuma cha pua nchini China, ilimaliza mazungumzo na wafanyabiashara wakubwa wa mawe ya madini ya chuma duniani, ambapo kilithibitishwa kiwango cha bei ya mawe ya madini ya chuma ya mwaka 2007, hii ni mara ya kwanza kwa kampuni za China kupata haki ya kupanga kiwango cha bei katika biashara kubwa ya malighafi duniani. 
  • China yahimiza ujenzi wa nyumba ndogo na za wastani ili kutatua tatizo la nyumba kwa wakazi wenye mapato ya chini
  •  2007/02/06
    Kutokana na maendeleo ya uchumi wa China na kuinuka kwa kiwango cha maisha ya watu, wananchi wa China wamekuwa na mahitaji makubwa ya nyumba
  • China yashiriki kwenye makubaliano ya kimataifa kuhusu utoaji wa hewa inayosababisha kuongezeka kwa joto duniani
  •  2007/01/30
    Katika miaka ya karibuni utoaji wa hewa inayosababisha kuongezeka kwa dunia kuwa joto imekuwa ikifuatiliwa na watu wa nchi mbalimbali. "Mkataba wa Kyoto", ambao ulianza kufanya kazi mwaka 2005 unaagiza kuwa nchi zilizoendelea zinatakiwa kupunguza utoaji wa hewa inayosababisha kuongezeka kwa joto duniani, lakini haujatoa maagizo kwa nchi zinazoendelea.
  • Ujenzi wa vijiji vipya vya ujamaa waendelezwa vizuri nchini China
  •  2007/01/23
    Mwaka 2006 ni mwaka ambao ujenzi wa vijiji vipya vya ujamaa nchini China ulianza. Katika mwaka huo wakulima wa China licha ya kufurahia kupata mavuno mazuri ya kilimo, pia walifurahishwa na zaidi na maendeleo yaliyopatikana katika ujenzi wa vijiji vipya.
  • Kilimo cha kisasa chabadilisha hali ya unyonge wa sehemu ya vijiji nchini China
  •  2007/01/16
    Kuanzia mwaka huu China itafanya ujenzi kamambe wa kujenga vijiji vipya kote nchini na kutoa ruzuku kubwa kwa ajili ya kuboresha zana za uzalishaji mazao na maisha ya wakulima ili kupunguza tofauti kati ya miji na vijiji. Kati ya kazi hizo, kazi ya kubadilisha kilimo cha jadi kilichopitwa na wakati na kuanzisha kilimo cha kisasa chenye ufanisi mzuri, ni moja ya kazi muhimu za kujenga vijiji vipya.
  • Ujenzi wa utaratibu wa sheria kwenye soko la mitaji wahimiza mabadiliko ya kihistoria kwenye soko la hisa
  •  2007/01/09
    Habari kutoka kamati ya usimamizi wa soko la hisa ya China zilisema, tangu "Sheria ya kampuni ya Jamhuri ya watu wa China" na "Sheria ya hisa ya Jamhuri ya watu wa China" zianze kutekelezwa tarehe 1 mwezi Januari mwaka 2006, ujenzi wa utaratibu wa sheria wa soko la mitaji wa China umepata maendeleo makubwa na kuhimiza mabadiliko ya kihistoria kwenye soko la hisa la China, sheria hizo zilirekebishwa na kupitishwa mwaka 2005.
  • Magari yenye hataza ya China yaoneshwa kwenye maonesho ya magari ya kimataifa ya Beijing
  •  2007/01/02
    Maonesho ya magari ya kimataifa ya mwaka 2006 ya Beijing yalifungwa tarehe 27 mwezi Desemba, vitu vilivyofuatiliwa sana na watu kwenye maonesho hayo ni magari mengi yenye hataza ya China. Magari hayo ya China yalichukua theluthi moja ya magari yote mapya yaliyooneshwa kwenye maonesho hayo
  • China yaingia katika kipindi kipya cha kufungua mlango
  •  2006/12/26
    Tarehe 11 mwezi Desemba ni siku ambayo China ilitimiza miaka 5 tangu China ijiunge na shirika la biashara duniani, WTO. Muda wa miaka 5 unamaanisha kumalizika kwa kipindi cha mpito cha kujiunga na WTO kwa China, ambapo inaonesha kuwa China imeingia kipindi kipya ya kufungua mlango kwa pande zote.
  • Ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na umoja wa nchi za Asia ya kusini mashariki waingia katika kipindi kizuri
  •  2006/12/19
    Mwaka huu miaka 15 imetimia tangu uhusiano wa mazungumzo kati ya China na umoja wa nchi za Asia ya kusini mashariki uanzishwe. Hivi karibuni viongozi wa China na nchi 10 za umoja wa Asia ya kusini mashariki walishiriki kwenye mkutano uliofanyika katika mji wa Nanning, mji mkuu wa mkoa unaojiendesha wa kabila la wazhuang, China, na kuweka mpango kamambe wa maendeleo katika siku za baadaye.
  • Ushirikiano kati ya kampuni binafsi na kampuni za kimataifa nchini China waendelezwa kwa kina
  •  2006/12/12
    Katika siku za karibuni kampuni binafsi nchini China zilikuwa na mazungumzo na kampuni kubwa za kimataifa kwenye mji wa Wenzhou, mkoani Zhejiang, sehemu ya kusini mashariki mwa China.
  • Idara za hifadhi za mazingira kuanzisha harakati za kuchunguza bidhaa zisizo na uchafuzi kwa mazingira
  •  2006/12/05
    Habari kutoka kituo cha uthibitishaji wa bidhaa za kijani cha idara kuu ya mazingira ya taifa zinasema, kamati ya uthibitishaji wa bidhaa zenye nembo ya hifadhi ya mazingira ya China itashirikisha na idara za viwanda
  • Uvumbuzi waleta mali
  •  2006/11/28
    Hivi sasa uvumbuzi unaambatana na maisha na kazi za watu. Uvumbuzi unaweza kuleta mali nyingi kwa watu, hivi sasa sekta ya uvumbuzi imekuwa sekta moja mpya inayofuatiliwa sana nchini China. Kampuni ya GOGO time iliyoanzishwa mwaka 2005 kwenye eneo la ustawishaji wa teknolojia la Zhongguancun, hivi sasa imekuwa mfano wa kuigwa kwa kampuni za wastani na ndogo za uvumbuzi mjini Beijing.
  • Sekta ya uzalishaji mitambo ya sehemu ya kaskazini mashariki mwa China yapata maendeleo ya kasi
  •  2006/11/21
    Mwaka 2004 China ilianza kutekeleza sera za kustawisha sehemu ya kaskazini mashariki mwa China, ikinuia kurejesha ustawi wa zamani kwa kituo hicho cha kazi za viwanda. Tangu kuanza kutekelezwa kwa sera hizo na kufanya marekebisho ya muundo wa uzalishaji mali katika miaka miwili iliyopita, maendeleo ya uchumi ya sehemu ya kaskazini mashariki yalipata nafasi nzuri, hususan sekta ya uzalishaji mitambo ilikuwa na maendeleo ya kasi.
  • Mustakabali mzuri wa ushirikiano wa nishati wa nchi za Asia ya mashariki
  •  2006/11/14
    Katika miaka ya karibuni, ongezeko la uchumi wa Asia ni kubwa zaidi kuliko kiwango cha wastani duniani, ambapo thamani ya biashara kati ya nchi za Asia ya mashariki zikiwemo China na Japan, pia inaongezeka kwa mfululizo.
  • Sehemu ya kusini magharibi mwa China yavutia uwekezaji kutoka nchi za Umoja wa Asia ya kusini mashariki
  •  2006/10/31
    Tokea miaka ya 70 ya karne iliyopita, wafanyabiashara wenye asili ya China wa nchi mbalimbali za Umoja wa Asia ya kusini mashariki wamekuwa chanzo muhimu cha uwekezaji kutoka nchi za kigeni nchini China, ambao wametoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya uchumi wa China.
  • Serikali ya China yaimarisha udhibiti wa kuhusu uzalishaji chakula
  •  2006/10/31
    Naibu mkurugenzi mkuu wa idara ya chakula ya serikali Bw. Qie Jianwei tarehe 25 mwezi Septemba kwenye mkutano wa 10 wa baraza la soko la chakula la China alisema, hivi sasa uzalishaji na usafirishaji chakula wa China umeingia kipindi kipya cha maendeleo, utaratibu wa usafirishaji chakula unaboreshwa hatua kwa hatua, mageuzi ya mashirika ya chakula ya taifa yanaendelezwa kwa kina na uwezo wa udhibiti wa mpango mkuu wa serikali kuu kuhusu uzalishaji chakula unaimarishwa hatua kwa hatua.
  • Beijing yahamisha viwanda vya kazi nzito
  •  2006/10/24
    Katika miaka ya karibuni Beijing imehamisha viwanda vingi vya kazi nzito ambavyo ni pamoja na kampuni ya chuma na chuma cha pua ya mji mkuu, kiwanda cha makaa ya mawe na kiwanda cha mitambo ya vyombo (machine tool).
  • Eneo la uchumi la ghuba ya kaskazini mwa mkoa wa Guangxi
  •  2006/10/17
    Sehemu ya magharibi mwa China ina mikoa na miji 12 kwa jumla, eneo lake ni kilomita za mraba milioni 6.85 likichukua asilimia 71.4 ya ardhi yote ya China, na ina idadi ya watu milioni 367. Sehemu ya magharibi ya China ina rasilimali nyingi na soko kubwa katika siku za baadaye.
  • Watu wapenda "wiki ya dhahabu"
  •  2006/10/10
    Mkurugenzi mtendaji wa ofisi inayoshughulikia mambo ya likizo ya serikali ambaye pia ni naibu mkurugenzi wa idara ya utalii ya China Bw. Wang Zhifa, tarehe 28 mwezi Septemba alipohojiwa na mwandishi wa habari alisema, katika mazingira ya hivi sasa ambayo utaratibu wa mapumziko haujakamilika.
    1 2 3 4