![]() Watford wamemtimua kocha Nigel Pearson zikiwa zimesalia mechi mbili pekee kabla ya kampeni za Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu kutamatika rasmi. |
![]() Ligi Kuu ya Kenya imepata nguvu mpya baada ya kampuni ya Bahati Nasibu ya Nigeria Bet King, kukubali kuifadhili Ligi hiyo kuanzia msimu ujao. Hatua hiyo imekuja baada ya Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) kufikia makubaliano na kampuni hiyo hapo jana. |
![]() Mshambuliaji Harry Kane alifikisha zaidi ya mabao 200 katika taaluma yake ya soka kwenye ngazi ya klabu baada ya kutikisa wavu mara moja na kusaidia Tottenham Hotspur kuwapepeta Newcastle United 3-1 katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) hapo jana. |
![]() Kitengo cha Maadili (AIU) cha Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF) kimempiga marufuku mtimkaji Alex Korio Oloitiptip kushiriki mashindano kwa miaka miwili kwa kukiuka kanuni zinazodhibiti matumizi ya pufya. |
![]() Imekuwa afueni kubwa kwa Manchester City baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Migogoro katika Michezo (CAS) kubatilisha maamuzi ya awali ya UEFA ambao wamewapiga miamba hao wa soka Uingereza marufuku ya kushiriki kipute cha Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) kwa kipindi cha misimu miwili. |
![]() Kocha wa mchezo wa Chess nchini Tanzania, Kara Louis ameelezea mashindano ya mchezo huo yaliyofanyika kwa njia ya mtandao yajulikanayo kama African Juniors 11 Team Battle yaliyohusisha nchi sita, kuwa ni mashindano mazuri yatakayowatangaza wachezaji wadogo. |
![]() BAADA ya kuifungia timu yake bao pekee kwenye ushindi walioupata dhidi ya Kagera Sugar juzi, kiungo mwenye 'mbwembwe' wa klabu ya Yanga, Bernard Morrison amesema hizo ni salamu kwa wapinzani wao |
![]() Wakati mechi ya michezo ya hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Federation (FA) inakaribia nahodha wa Yanga, Juma Abdul, amewatoa hofu mashabiki wa Yanga na kuwataka kuwa na furaha kwenye kipindi hiki ambacho wanafanya maandalizi makubwa kuelekea kwenye mchezo dhidi ya watani wao wa jadi Simba. |
![]() Nembo ya namba tatu iliyopo katika jezi mpya za Chelsea, zinaweza kutafsiriwa kama ni mkosi baada ya timu hiyo kuchapwa mabao 3-2 na West Ham ikizitumia kwa mara ya kwanza juzi. |
![]() Kiungo wa Manchester City Leroy Sane, inaelezwa kuwa amemaliza utaratibu wote na Klabu ya Bayern Munich ili aitumikie timu hiyo msimu ujao. |
![]() Nyota wa ndani ya Klabu ya Barcelona Lionel Messi, usiku wa kuamika leo alifunga bao moja kwenye sare ya kufungana mabao 2-2 na Atletico Madrid Uwanja wa Nou Camp kwenye La Liga na kufikisha jumla ya mabao 700. |
![]() Klabu ya Valencia ya Hispania imeamua kumfuta kazi kocha wao Albert Celades , 44, baada ya kuwa na mfululizo wa matokeo mabovu. |
![]() Liverpool walinyakua ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kwa mara ya kwanza baada ya miaka 30 jana Juni 25 kufuatia ushindi wa 2-1 uliosajiliwa na Chelsea dhidi ya mabingwa watetezi Manchester City. |
![]() Mshambuliaji matata wa Tottenham Hotspur, Harry Kane amesema kwamba analenga kuwa mchezaji wa tatu baada ya Alan Shearer na Wayne Rooney kufunga jumla ya mabao 200 katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). |
![]() Chama cha Mchezo wa Magongo Tanzania (THA) kimetangaza kuwa mashindano ya Kombe la Nyerere yatafanyika Oktoba mwaka huu mjini Moshi, Kilimanjaro. |
![]() Nyota wa mchezo wa mieleka WWE, Mark Calaway maarufu kama The Undertaker ametangaza kustaafu kwake baada ya kudai kuwa hana lengo lingine la kutimiza katika mchezo huo. |
![]() Klabu ya Liverpool imepanga kumsajili nyota wa Paris Saint-Germain Kylian Mbappe kwa kubadilishana na mchezaji wao, Sadio Mane na kitita cha paundi milioni 200. |
![]() Mabingwa wa Ligi Kuu ya Kenya, Gor Mahia na AFC Leopards wameingia katika mkataba mpya na kampuni ya mchezo wa bahati nasibu Bet High Kenya, chini ya chapa yao ya BetSafe. |
![]() Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Sepp Blatter anachunguzwa kwa matumizi mabaya ya mkopo wa Dola milioni moja ambao FIFA unadaiwa kulipatia Shirikisho la Soka la Trinidad & Tobago 2010. |
![]() Matumaini ya Arsenal ya kumaliza miongoni mwa vilabu nne bora ilipata pigo kufuatia ushinde wa 3-0 kwa Man City ugani Etihad. |
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |