Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia

  • Kukunja karatasi
  •  2005/02/04
        Karatasi moja ya kawaida huweza kukunjwa na kuonekana kuwa mnyama mdogo anayeonekana kama yu hai, baada ya Bwana Liu Xiaoyi kuikunjakunja kwa mikono yake hodari. Vipepeo, mavunjajungu, samaki wa rangi ya dhahabu, mbuzi, tembo na swala hupendaza sana kutokana na kutengenezwa kwao kwa ufundi au kwa maumbo yao. Kwa vile ustadi wa Bwana Liu wa kukunja karatasi ni mkubwa sana, hivyo habari zake ziliandikwa katika kitabu cha Watu Maarufu wa Kimataifa tokeo la mwaka 1987-1988 kilichotungwa na Kampuni ya Uchapishaji ya Ulaya huko Uingereza.
  • Ukataji wa karatasi
  •  2004/10/22
    "Maua ya plum ni kiboko ya maua: yanachanua hata siku za baridi kali. Kunguru(magpie) wawili wanaimba kwenye tawi; wanatutakia furaha ya mwaka mpya."
  • Ubandikaji Karatasi
  •  2004/07/01
    Zhizha maana yake ni taswira zilizobandikwa kwa karatasi, nazo zinatengenezwa kwa karatasi za rangi anuwai, vipande vidogo vya mianzi, matete na seng'enge. Hatua za kutengeneza ni hivi: kwanza kuunda miimo yake kwa vipande vidogo vya mianzi, mabua ya matete na seng'enge, kisha kubandika karatasi za rangi zilizokatwakatwa na kupambwapambwa, mwishowe hutokea taswira mbalimbali za kuvutia. Ikiwa ni taswira ya mtu hufunga kichwa cha udongo, kutia rangi za uso na pia kumshikisha ala za vita mikononi mwake.
  • Sanaa ya ukataji karatasi kwa kuigiza vyombo vya kale
  •  2004/03/16
    Vyombo vya kale vya kauri vya China vyenye historia ya miaka 4,000 kuanzia kipindi cha umajumui hadi mwisho wa enzi ya Qing, vinajulikana kwa umakini wake wa ufinyanzi, uzuri wa maumbo, upendezaji macho wa mabombwe na uangavu wa rangi. Baadhi ya vyombo hivyo vyenye thamani kubwa vinahifadhiwa kizazi baada ya kizaza, na kurithiwa mpaka leo, kwa mfano gudulia la kauri nyeupe na buluu la enzi ya Yuan lenye mabombwe ya "Xiao He anamkimbilia Han Xin usiku wa mbalamwezi" na mtungi wa kauri nyeupe na buluu wa enzi ya Ming wenye mabombwe ya "Chrysanthemum za kipupwe na ndege aimbae" ndio vyombo viwili vilivyorithiwa mpaka leo.
    More>>
    More>>