• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shirika kuu la Utangazaji la China CMG latangaza habari kumi kubwa za kimataifa kwa mwaka 2019

  (GMT+08:00) 2019-12-31 09:44:29
  Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG Jumamosi lilitangaza habari kumi kubwa za kimataifa zilizofuatiliwa zaidi katika mwaka 2019.

  1. Rais Xi Jinping wa China alifanya ziara saba katika nchi za nje na kuhudhuria shughuli nne kubwa za kidiplomasia zilizofanyika China, na kupendekeza kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja

  Mwaka 2019, rais Xi Jinping wa China alifanya ziara saba katika nchi 12 za mabara ya Asia, Ulaya na Latin Amerika, na kuhudhuria mikutano mbalimbali ya kimataifa ukiwemo Mkutano wa Baraza la Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai SCO, Mkutano wa kilele wa hatua za kujenga ushirikiano na uaminifu barani Asia CICA, Mkutano wa viongozi wa kundi la nchi 20 (G20) na Mkutano wa kilele wa Nchi za BRICS. Mwaka 2019, Rais Xi pia aliongoza shughuli nne kubwa za kidiplomasia zilizofanyika nchini China, ambazo ni mkutano wa pili wa kilele wa Baraza la ushirikiano wa kimataifa wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", Maonesho ya Kimataifa ya Bustani na Kilimo cha Maua ya Beijing, Mkutano wa Mazungumzo kati ya Staarabu za Asia na Maonesho ya Pili ya Kimataifa ya bidhaa zinazoagizwa na China kutoka nje CIIE.

  Kwenye shughuli hizo za kidiplomasia, rais Xi Jinping alifafanua uzoefu wa mafanikio ya China, kupendekeza kujenga Jumuiya ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja, na kutoa ufumbuzi wa China unaokidhi matarajio ya jumuiya ya kimataifa na kuendana na maslahi ya pamoja ya kila upande, ambao unaelekeza juhudi za kukamilisha usimamizi wa dunia, na kubeba wajibu wa China kama nchi kubwa inayowajibika.


  1  2  3  4  5  6  7  8  9  10  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako