• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shirika kuu la Utangazaji la China CMG latangaza habari kumi kubwa za kimataifa kwa mwaka 2019

  (GMT+08:00) 2019-12-31 09:44:29

  3. Marekani na Russia zajitoa kwenye Mkataba wa Silaha za Nyuklia za Masafa ya Kati INF

  Wizara ya mambo ya nje ya Marekani mwezi Februari ilitangaza kusitisha utekelezaji wake wa Mkataba wa Silaha za Nyuklia za Masafa ya Kati INF. Mara baadaye Russia pia ilitangaza kusitisha utekelezaji wa mkataba huo. Agosti 2, Marekani na Russia zilitangaza kwa nyakati tofauti kuwa Mkataba wa INF hauna nguvu tena. Agosti 18 Marekani ilifanya jaribio la kombora kutoka ardhini. Rais Putin wa Russia akailaumu Marekani kuwa na mpango wa kujitoa INF kwa muda mrefu.

  Kwa mujibu wa mkataba wa INF, Marekani na Russia haziruhusiwi kumiliki, kuzalisha au kufanya majaribio ya makombora ya masafa kati ya kilomita 500 hadi 5,500. Kufutwa kwa INF kumetoa changamoto kubwa kwa mfumo wa kimataifa wa udhibiti wa silaha ulioanzishwa baada ya Vita Baridi.


  1  2  3  4  5  6  7  8  9  10  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako