• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika kuu la Utangazaji la China CMG latangaza habari kumi kubwa za kimataifa kwa mwaka 2019

    (GMT+08:00) 2019-12-31 09:44:29

    4. Brexit yakabiliwa na changamoto

    Uingereza ilipanga kujitoa Umoja wa Ulaya Machi 29, lakini kutokana na makubaliano ya Brexit kushindwa kupitishwa bungeni, aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May alilazimika kujiuzulu Juni 7. Baada ya Bw. Boris Johnson kurithi uongozi wa chama cha kihafidhina na uwaziri mkuu, alifanikiwa kuahirisha tarehe ya Brexit kutoka Oktoba 31 mwaka 2019 hadi kufikia Januari 31 mwaka 2020. Bw. Johnson alishinda uchaguzi uliofanyika mwezi Desemba, na kuhimiza baraza la makabwela kupitisha miswada husika ya sheria Desemba 20, ili kuhakikisha Uingereza inajitoa Umoja wa Ulaya mwishoni mwa Januari mwakani kama ilivyokubaliwa. Mchakato wa Brexit uliokwama ulitoa pigo kubwa kwa uchumi wa Uingereza, na pia kutoa changamoto kubwa kwa mchakato wa mafungamano ya Ulaya.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  10  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako