• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shirika kuu la Utangazaji la China CMG latangaza habari kumi kubwa za kimataifa kwa mwaka 2019

  (GMT+08:00) 2019-12-31 09:44:29

  6. Binadamu wapiga picha ya kwanza ya Shimo Jeusi, ambalo linaweza kuthibitisha utabiri wa Einstein

  Tarehe 10 mwezi Aprili, wanafalaki wa nchi kadhaa ikiwemo China wameonesha picha ya kwanza ya Shimo Jeusi (Black Hole) kwa wakati mmoja. Mradi wa EHT ulioshirikisha zaidi ya wanasayansi 200 wa nchi mbalimbali duniani ulitumia zaidi ya miaka 10, na mwishowe kupata picha hiyo katika vituo vinane vya kuchunguzia anga za juu vilivyoko kwenye mabara manne duniani. Shimo Jeusi hilo liko miaka milioni 55 ya mwanga mbali na dunia, na uzito wake ni mara bilioni 6.5 ya Jua.

  Shimo Jeusi ni eneo kwenye anga za juu lenye ukubwa mdogo na uzito mkubwa lililotabiriwa na mwanasayansi maarufu Albert Einstein, lina mvuto mkubwa na hata mwanga hauwezi kupenya. Hata hivyo binadamu walishindwa kuliangalia moja kwa moja, lakini kutokana na maendeleo ya teknolojia na ushirikiano wa wanasayansi duniani, hatimaye binadamu wamefungua dirisha jipya la kuchunguza Shimo Jeusi.


  1  2  3  4  5  6  7  8  9  10  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako