• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika kuu la Utangazaji la China CMG latangaza habari kumi kubwa za kimataifa kwa mwaka 2019

    (GMT+08:00) 2019-12-31 09:44:29

    5. Jeshi la serikali la Syria ladhibiti asilimia 85 ya ardhi ya nchi hiyo, siasa ya kanda ya Mashariki ya Kati yana hali mpya

    Tarehe 22 Oktoba, rais Vladimr Putin wa Russia na mwenzake wa Uturuki Recep Erdogan walifanya mazungumzo, na kufikia makubaliano kuhusu hali ya Syria. Kutokana na makubaliano hayo, pande hizo zilianzisha eneo salama katika mpaka kati ya Uturuki na Syria. Hadi sasa jeshi la serikali la Syria limekalia sehemu kadhaa kaskazini, na kudhibiti asilimia 85 ya ardhi ya nchi hiyo. Tarehe 30 mwezi Oktoba, kamati ya katiba ya Syria iliyoundwa na serikali na makundi ya upinzani ilianzishwa mjini Geneva, ili kuhimiza mchakato wa maafikiano ya kisiasa kupitia mageuzi ya katiba. Mabadiliko ya hali ya Syria yanaonesha mivutano kati ya Russia, Marekani, Uturuki na Iran, na ushawishi wa Russia umeimarika. Wakati huohuo, Marekani imeongeza shinikizo dhidi ya Iran, na suala la nyuklia la Iran limekwama tena.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  10  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako