• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shirika kuu la Utangazaji la China CMG latangaza habari kumi kubwa za kimataifa kwa mwaka 2019

  (GMT+08:00) 2019-12-31 09:44:29

  7. Ajali ya Ndege ya Ethiopia yaua watu 157, ndege zote za abiria aina ya Boeing 737 MAX yasimamishwa kuruka

  Tarehe 10 mwezi Machi, ndege moja ya abiria aina ya Boeing 737MAX iliyomilikiwa na Shirika la Ndege la Ethiopia ilianguka baada ya kuruka kutoka mji wa Addis Ababa, Ethiopia, na kusababisha vifo vya watu 157. Hii ni ajali kubwa ya pili ya ndege ya aina hiyo baada ya ajali ya ndege ya Shirika la ndege la Indonesia iliyotokea mwezi Oktoba mwaka jana.

  Kutokana na ajali hizo, nchi zote duniani zilisimamisha matumizi ya ndege aina ya Boeing 737MAX. Mamlaka ya usafiri wa anga ya Marekani ililaumiwa kukabidhi kazi za kuthibitisha hati ya usalama wa kuruka kwa ndege (Airworthiness Certificate) kwa mashirika ya kutengeneza ndege. Baadaye mamlaka hiyo ilikatisha hati hiyo kwa ndege aina ya Boeing 737MAX. Shirika la Boeing limetangaza kusimamisha uzalishaji wa ndege hiyo kuanzia Januari mwaka ujao, na meneja mkuu wake amelazimika kujiuzulu.


  1  2  3  4  5  6  7  8  9  10  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako